Zinazobamba

TCRA WAZINDUA ZOEZI LA UHAKIKI NA USAJIRI WA LAINI ZA SIMU,WATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUHAKIKI LAINI ZAO


PROF.JOHN NKOMA AKIFAFANUA JAMBO KATIKA MKUTANO ULIOWAKUTANISHA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA NIDA,JESHI LA POLISI ILI KUZINDUA ZOEZI LA KUHAKIKI LAINI ZA SIMU KWA NJIA YA TEKLOJIA MPYA YA ADROID KYC. NKOMA ALISEMA TAKRIBANI LAINI 32 MILIONI ZIMESAJILIWA LAKINI LAINI NYINGI TAARIFA ZAKE ZINACHANGAMOTo. KATIKATI NI MWENYEKITI WA UMOJA WA MAKAMPUNI YA MAWASILIANO   TANZANIA(MOAT) BW. LENE MEZA
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa mamlaka ya vitambulisho NIDA Bw. Thomas William akielezea jambo kuhusu umuhimu wa kitambulisho cha taifa na zoezi la kuhakiki laini za simu. Wiliam alisema vitambulisho vya taifa vina taarifa za kuaminika na sahihi za kila mkazi wa Tanzania na ndio sababu inapendkezwa kutimika katika zoezi hili.

Na SelemaniMagali.

Mamlaka ya mawasiliana Tcra imetangaza kuzindua rasmi zoezi la kuhakiki na kusajiri laini za simu kwa kutumia mfumo mpya kabisa wa kidijitali Kupitia Smart Phone kwa Programu ya KYC 
 Akitangaza kuanza kwa zoezi hilo (validation of sim card) Prof. Nkoma alisema wananchi wanapaswa kujitokeza kwenda kuhakiki laini zao ili  kuendelea kujipatia huduma zilizo bora kupitia laini zao ambazo zimesajiriwa kihalali.
Alisema zoezi hilo litaendeshwa kwa njia ya Mtandao, ambapo mawakala watatumia simu ya mkononi aia ya smatphone ili kujaza taarifa za uhakiki wa laini pamoja na usajiri ambao vitaenda sambamba.
Aliongeza kusema ujio wa zoezi hilo ni la kawaida ambapo hata benki kuu ya Tanzania BOT iliwahi kuagiza benki mbalimbali hapa nchini kufanya uhakiki wa akaunti za wateja wao ili kuwa na taarifa muhumu za wateja
Akizungumzia jinsi zoezi litakavyo tekelezwa, Prof Nkoma alisema makampuni ya simu watatumia mawakala wao kusajiri na kuhakiki wateja ambao tayari wamesajiriwaa kwa kutumia smatphone ambazo zitagawiwa kwao ili kutekeleza kazi hiyo muhimu.
Alisema mteja atalazimika kuwa na kitambulisho cha taifa ili afanyiwe uhakiki,na kwamba kwa wale ambao kwa kiasi kikubwa hawana wafanye jitihada ya kutafuta kitambulisho hicho ambacho kwa sasa alidai kinapatikana ndani ya siku saba.
Teknolojia hiyo mpya inauwezo wa kutambua kitambulisho bandia, uwezo wa kupiga picha, kupiga picha ya kitambulisho, kutia saini zote mbili ya mteja na wakala, na kujaza taarifa muhimu za mteja, na kwamba inafanya kazi hizo kwa haraka na uhakika.


No comments