MTANGAZA NIA URAIS CCM APIGWA MAKONDE NA "TEAM LOWASSA",SOMA HAPO KUJUA

Dr. Kalokola akionesha briefcase lenye fomu za kutafutia wadhamini mjini Dodoma
Huyo mzee anaitwa Muzammil Mussa Kalokola ni Mchumi na mmoja wa waliochukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka huu 2015, kutoka Jiji la Tanga, na yupo anazunguka akitafuta wadhamini, kama wanavyo fanya Wengine walio chukua fomu.
Hili tukio Lilitokea alipoenda kwenye Mkutano wa Mh. Edward Lowassa, alipokua Tanga na fomu za kuomba udhamini, Ndio wakamtenda hivyo.
Nalaani hiki kitendo walichofanya green guard kwani hata kama walikua hamtaki, wangemuondoa kistaarabu tu kuliko walivyomdhalilisha. Mbona sehemu nyingine Wagombea urais wakikutana wanasalimiana? Lowassa alipokutana na Samwel Sitaa Walisalimiana wakakaa wakaongea, kwanini huyu aamulishe kupigwa?
Kumbuka Dr. Muzamil Kalokola, ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kuhifadhi Mawazo ya Mwalimu Nyerere alifungua shauri katika Mahakama Kuu jijini Tanga dhidi ya Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba akidai Mahakama kutamka kwamba uteuzi wa wabubnge wa Bunge la Katiba haukufuata misingi mikuu ya demokrasia kitu ambacho kimeathiri uhalali wa Bunge hilo. Kesi hiyo ya madai namba 02/2014, ilifunguliwa Februari 17.2014.
Washtakiwa katika kesi hiyo iliyofunguliwa kwa stakabadhi ya malipo ya Serikali namba 49803745, ni Waziri wa Sheria na Katiba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)kipindi hicho Frederick Werema) na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo Mwenyekiti wake ni Jaji Mstaafu, Joseph Warioba.
Vilevile aliiomba mahakama kutupilia mbali uteuzi wa wajumbe wa Bunge hilo kwa kutofuata misingi ya demokrasia na uwakilishi. Mwanaharakati huyo pia alingumzia posho za wabunge hao na kuitaka mahakama kuzikataa kwa sababu zitakua mzigo kwa uchumi kwa taifa.
Dr. Kalokola Mwaka huu naye aliamua kujitosa Kwenye Urais ili Kusimamia Misingi ya Muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
No comments
Post a Comment