HATIMAYE SASA,MZEE YUSUPH KUGOMBANIA UBUNGE,SOMA HAPA KUJUA JIMBO GANI
PICHANI NI MZEE YUSUPH PICHA NA MAKTABA |
MSANII wa Muziki
wa Taarabu kutoka Bendi ya Jahazi Modern Taarabu ,Mzee Yusuph anatalajia
kugombania Ubunge kupitia Jimbo la Fuoni lilopo Unguja kwa kupitia CCM,Mtandao
huu umedokezwa,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Mzee Yusuph ambaye ni Mwazilishi wa
Taarabu za Mfumo wa Modern nchini atalajia kuchukua fomu mda wowote kutoka sasa
na kumpiku Mbunge wa sasa wa Jimbo hilo,Said Mussa Zuberi.
Kwa Mujibu wa Mzee Yusuph ambaye pia ni Mmiliki wa Bendi ya Jahazi,anasema
lengo la yeye kugombani Ubunge Jimbo
hilo ni kutaka kuwaleta maendeleo kwa Wananchi wa Fuoni pamoja na Wazanzibari
kwa Ujumla..
Pamoja na hayo Msanii huyo wa Zamani wa
Bendi ya Zanzibar Melody Taarabu
amewataka Wananchi wa Jimbo hilo kumuunga mkono kwani yeye ni mtu sahihi ambaye
anaweza kuwaleta Maendeleo Makubwa.
Kuibuka kwa Mzee Yusuph kunazidisha idadi ya
Wasanii wa Muziki ambao wanatarajia kugombania nafasi mbali mbali za uongozi kwenye uchaguzi Mkuu wa hapo baadae mwaka huu, baada ya Hivi Karibuni Msanii wa Bongo fleva,Profesa Jay kutangaza Rasmi
kuombania Ubunge Jimbo la Mikumi kupitia muunganiko wa Vyama vikuu vya Upinzani
vinavyounda UKAWA.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni