Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO-KAMBI YA LOWASSA YAKATA TAMAA,SASA KUKIMBILIA ACT-WAZALENDO,NI ILE YA "TEAM LOWASSA",SOMA HAPO KUJUA



WAKATI zikiwa zimebaki siku ishirini na mbili kufika tarehe 11 mwezi wa saba ili chama cha mapinduzi CCM  kimteue mgombea wa Nafasi ya Urais ndani ya Chama hicho kwenye uchaguzi mkuu hapo baadae mwaka huu,Kambi ya Kada wake amayeutaka Urais Edward Lowassa (pichani) imeanza kukata tamaa kwamba mgombea huyo kupita na sasa wamejipanga kutimkia ACT Wazalendo.Mtandao huu unafahamu.Aaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
         Kambi hiyo ya Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli ni ile inayoitwa "Team Lowassa"ambayo imeunda kundi linaloiwa "For you movement" ambayo ilianzishwa kwa malengo mbali mbali.
             Malengo hayo ikiwemo kumsafisha Lowassa kwenye Kashfa mbali mbali zinazomkabili ikiwemo ile ya Ufisadi wa kutisha kwenye Kampuni Tata ya Richmound pamoja na kumnadi kwenye mitandao mbali mbali  ya Kijamii ili kumfanya akubalike kwa jamii.
             Taarifa ambazo mtandao huu umezipata kutoka ndani ya Kambi ya Lowassa inasema kwa sasa ni kama kambi hiyo imeshaanza kukata tamaa kama Mgombea wao atapitishwa na Kamati kuu ya Chama cha mapinduzi CCM pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC)kwa kile wanachokiona kutokubalika na viongozi waandamizi wa CCM.
          "Watu wengi kwenye Kambi hii wameshaona mzee hana nafasi tena kwenye Chama, maana hata ukiangalia kila mgombea akitangaza nia ya Urais anamponda lowassa wakati kuna wagombea wengi wametangaza nia harafu-"
 "Huku ukizingatia hawa wanaomponda wengine ni wajumbe kwenye sehemu ya Maamuzi ndani ya CCM sasa unategemea nini,kusema kweli wengi wetu tumeanza kukata tamaa na kutafuta upenyo kwengine na lazima tutimkie kwengine lazima CCM izizime"amesema Kiongozi huyo wa Kambi ya lowassa.
  Alipoulizwa na Mwandishi wa Mtandao huu, kama endapo Lowassa asipopita ni chama gani wanataka  kwenda  ambapo alisema  "Wengi wetu tumeamua kwenda ACT-Wazalendo tukaongeze nguvu tu maana tumeona Sera zake zinaendana na Misimamo yetu,nakuhakikishia Jamii itazimima:|
 Ameongeza kuwa kwa kusema "Hatuwezi kwenda UKAWA kutokana na Misimamo yao ilivyo,nakuhakikishia Lazima tushangaze nchi,CCM ya leo imekuwa ya Kibabe sana watu wachache (anataja Jina) ndio wakiongoze chama kama cha kwao"

1 comment

Mbele said...

Lowasa huyu huyu amekuwa akisema kuwa haondoki CCM. Sasa vipi?