Zinazobamba

HIVI NDIVYO KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU KILIVYOWAFUNDA WANAHABARI WA DAR


Mkurugenzi mkuu wa kituo cha sheria na haki za Binadamu Bi Kijjo Bisimba akifungua mkutano kwa waandishi wa habari kuhusu hali ya haki za binamu nchini. Mkutano huo ulilenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa Jiji la Dareslaam ili waweze kulipoti vyema taarifa zinahusu haki za bidam, Kijo Bisimba aliwataka waandishi wa habari kulipoti haki za binadam kwa weledi wao wote ili kuibua haki ambazo zinakandamizwa na watu iwe kwa sababu za pesa zao ama ujirani walionao.

Kituo cha sheria na haki za Binadamu mapema hiyo jana kimewajengea uwezo waandishi wa habari zinazohusiana na haki za binadamu ili waandishi hao waweze kuripoti habari amabazo wanauhakika nazo tena bila kumuonea mtu,
Akifungua mkutano huo uliojumuisha waandishi nguli katika tasnia ya habari hapa nchini, Mkurugenzi wa kituo hicho amewataka waandishi wa habari za haki za binadamu wawe makini katika mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kuibua haki ambazo zinakandamizwa na ambazo hajipewa kipaumbele ili wanachi waweze kupatiwa haki hizo kwa wakati kutoka kwa watu wenye mamlaka.
Mkurugenzi huyo amewataka wanahabari hao kuwafanya kazi zao kwa weledi na kuacha kupokea kitu kidogo ili kuficha haki za walalahoi ambao nao wanahaki ya kusikika,
Kumekuwa na tabia ya waandishi wa habari kuchukua kitu kidogo lakini jua kwamba kitendo cha kuchukua rushwa ya 100,000 huku anayekupa akifaidika kwa mamilioni ya shilingi kinakudhalilisha wewe na taaruma yako,
Naona ni vyema sasa mkaacha tabia ya kupokea mirungura ili kuuficha ukweli, kufanya hivyo ni kukandamiza haki za binadam. aliongeza Bi. Kijjo Bissimba.
Aidha katika mkutano huo kulikuwa na mada mbalimbali ambazo ziliwasilishwa ambapo, lakini moja ya mada ambayo ilikuwa na mjadala mpana ni kutoka Kwa Dada Anna Henga ambaye aliwafungua waandishi wa habari kuhusu haki ambazo zilitakiwa kuwepo katika katiba pendekezwa lakini hazikupata fursa.
Licha ya haki ambazo hazimo katika katiba pendekezwa, pia mwanasheria huyo ameowaonyesha waandishi jinsi katiba inayopendekezwa ilivyolazimishwa, na kuhoji kunaulazima gani wa katiba hiyo kuendelea kupigiwa kura ya moani huku katiba yenyewe ikiwa siyo shirikishi??????


Emelda Urio katika mafunzo na waandishi wa habari , Kituo cha sheria na haki za binadamu waliendesha semina ya siku moja kwa waandishi wa habari, mafunzo ambayo yalilenga kuwajengea uwezo waandishi ili kuweza kulipoti vema habari zinahusu haki za binadam, katika mafunzo hayo waandishi mbalimbali toka vyombo vya habari walihudhuria na kujionea wenyewe jinsi haki za binadamu zinavyokandamizwa hapa nchini.




Displaying DSC00922.JPG
Mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za Binadam Harold Sungusia akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu namna haki za binadamu zinakandamizwa katika Ttaifa la Tanzania. Ametoa mifano ya kipigo alichopata mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF na kipigo ambapo walishushiwa waandishi wa habari siku mbowe alipokuwa anaenda makao makuu ya polisi jijini Daresalaam, Ametumia jukwaa hilo kubainisha mambo mengi ambapo Fullhabari itakuletea makala yake hivi karibuni.


mwisho

Hakuna maoni