Zinazobamba

UFAFANUZI KUHUSU MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014 HUU HAPA



Katika Mkutano wake wa 102 uliofanyika tarehe 04/11/2014, Baraza la Mitihani la Tanzania liliidhinisha kutangazwa kwa matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ulifanyika kuanzia tarehe 10 hadi 11 Septemba, 2014.  Watahiniwa walifanya mtihani huo kwa kutumia Karatasi Maalum za “Optical Mark Reader- OMR” ambazo zilisahihishwa kwa kutumia Mfumo wa kompyuta.  Matumizi ya teknolojia ya OMR kwenye Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi yalianza mwaka 2012.

2.0USAJILI WA WATAHINIWA

Jumla watahiniwa  808,085 wa Shule za Msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 429,624 sawa na asilimia 53.17 na wavulana 378,461 sawa na asilimia 46.83.  Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 691 walikuwa ni wenye uono hafifu, watahiniwa 87 walikuwa ni wasioona, watahiniwa 374 wenye matatizo ya kusikia, watahiniwa 252 wenye mtindio wa ubongo na watahiniwa 27 wenye ulemavu zaidi ya mmoja.

Watahiniwa 792,122 sawa na asilimia 98.02 ya waliosajiliwa walifanya mtihani.  Kati yao wasichana walikuwa 422,625 sawa na asilimia 98.37 na wavulana walikuwa 369,497 sawa na asilimia 97.63.  Watahiniwa 15,963 sawa na asilimia 1.98  hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo utoro na ugonjwa.  Kati yao wasichana ni 6,999 sawa na asilimia 1.63 na wavulana ni 8,964 sawa na asilimia 2.37.

3.0MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2014

3.1Ufaulu kwa ujumla

Jumla ya watahiniwa 451,392  kati  ya  792,118 waliofanya mtihani huo  wamepata  alama  100  au zaidi katika alama 250. Idadi hii ni sawa na asilimia  56.99 . Kati yao wasichana ni 226,483   ambao ni sawa na asilimia 53.59 na wavulana ni 224,909   sawa na asilimia 60.87. Miongoni mwa watahiniwa waliofaulu wamo wenye ulemavu 795 (wasichana 355 ambao ni sawa  na asilimia 44.65 na wavulana 440 ambao ni sawa na asilimia 55.35 ya watahiniwa wote wenye ulemavu waliofanya mtihani). Mwaka 2013 asilimia ya watahiniwa walipata alama 100 au zaidi   ilikuwa 50.61, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 6.38. 


5.0WATAHINIWA WALIOPATA ALAMA ZA JUU KATIKA MASOMO

Wapo watahiniwa walioweza kufaulu kwa kupata alama 50/50 katika baadhi ya masomo ambapo English Language walikuwa 7,600, Kiswahili 32  na Hisabati 34. Ingawa  somo la Hisabati lina  ufaulu wa chini zaidi kuliko masomo yote, watahiniwa 34 wamepata alama 50/50  katika somo hilo ambapo kati yao Wasichana ni 08  na Wavualana ni 26  

7.0WATAHINIWA WALIOFUTIWA MATOKEO

Baraza la Mitihani la Tanzania limefuta matokeo yote ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE), 2014 ya mtahiniwa 01 aliyebainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo. Idadi hii ni ndogo ikilinganishwa na watahiniwa 13 waliofutiwa matokeo yao mwaka 2013 kwa sababu za udanganyifu.

Baraza linachukua fursa hii kuzipongeza sana Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa, Wilaya na walimu wote waliosimamia mitihani hii kwa kuzingatia ipasavyo Kanuni za Usimamizi wa Mitihani ya Taifa. Aidha, Baraza linawapongeza kwa dhati watahiniwa wote waliofanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi, 2014 kwa kutojihusisha na udanganyifu katika mitihani.

8.0HITIMISHO

Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi, 2014 yamewekwa  kwenye tovuti za Baraza  la Mitihani, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ili kila mtahiniwa aweze kuona matokeo yake. Tovuti hizo ni,

www.matokeo.necta.go.tz,
www.necta.go.tz au www.moe.go.tz
www.pmoralg.go.tz

Baraza la Mitihani la Tanzania   litawasilisha Matokeo hayo kwenye Mamlaka zinazohusika ili zifanye uchaguzi wa watahiniwa wa kujiunga na elimu ya Sekondari. Hivyo,  matokeo ya uchaguzi wa watahiniwa wa kujiunga  na Kidato cha Kwanza yatatangazwa na Mamlaka husika mara baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika.


Dkt. Charles E. Msonde
        KATIBU MTENDAJI










-->
  1. MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2014

    1. Ufaulu kwa ujumla

Jumla ya watahiniwa 451,392 kati ya 792,118 waliofanya mtihani huo wamepata alama 100 au zaidi katika alama 250. Idadi hii ni sawa na asilimia 56.99 . Kati yao wasichana ni 226,483 ambao ni sawa na asilimia 53.59 na wavulana ni 224,909 sawa na asilimia 60.87. Miongoni mwa watahiniwa waliofaulu wamo wenye ulemavu 795 (wasichana 355 ambao ni sawa na asilimia 44.65 na wavulana 440 ambao ni sawa na asilimia 55.35 ya watahiniwa wote wenye ulemavu waliofanya mtihani). Mwaka 2013 asilimia ya watahiniwa walipata alama 100 au zaidi ilikuwa 50.61, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 6.38.

Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja mbalimbali umeainishwa katika jedwali lifuatalo:

Daraja
Wavulana
Wasichana
Jumla
Idadi
Asilimia
Idadi
Asilimia
Idadi
Asilimia
A
6,378
1.73
3,953
0.94
10,331
1.30
B
55,460
15.01
43,329
10.25
98,789
12.47
C
163,071
44.13
179,201
42.40
342,272
43.21
A-C
224,909
60.87
226,483
53.59
451,392
56.99
D
135,242
36.60
186,697
44.18
321,939
40.64
E
9,346
2.53
9,441
2.23
18,787
2.37


    1. Ufaulu Kimasomo

Takwimu za matokeo zinaonesha kuwa ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 0.64 na 8.94 ikilinganishwa na mwaka 2013. Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambapo ufaulu ni asilimia 69.70 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Hisabati lenye ufaulu wa asilimia 37.56. Mchanganuo zaidi katika ufaulu wa masomo umeainishwa katika jedwali lifuatalo:

SUBJECT NAME
YEAR
CLEAN
PASSED (A-C)
GRADE D
GRADE E
KISWAHILI
2013
844,704
583,348
69.06
207,635
24.58
53,721
6.36
2014
791,924
552,003
69.70
198,993
25.13
40,928
5.17
KIINGEREZA
2013
844,678
300,001
35.52
437,695
51.82
106,982
12.67
2014
791,910
307,613
38.84
431,163
54.45
53,134
6.71
MAARIFA YA JAMII
2013
844,708
447,657
53.00
347,014
41.08
50,037
5.92
2014
791,938
454,043
57.33
296,592
37.45
41,303
5.22
HISABATI
2013
844,690
241,741
28.62
452,937
53.62
150,012
17.76
2014
791,869
297,411
37.56
387,489
48.93
106,969
13.51
SAYANSI
2013
844,570
401,059
47.49
378,834
44.86
64,677
7.66
2014
791,932
434,679
54.89
297,167
37.52
60,086
7.59

  1. SHULE KUMI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI

Shule 10 bora Kitaifa katika PSLE 2014 zimeainishwa katika jedwali lifuatalo

NAMBA JINA LA SHULE
IDADI
MKOA
NAFASI
PS0904095 TWIBHOKI
33
MARA
1
PS1303065 MUGINI
40
MWANZA
2
PS1307121 PEACELAND
17
MWANZA
3
PS1304001 ALLIANCE
25
MWANZA
4
PS1701035 KWEMA
50
SHINYANGA
5
PS0501188 ST SEVERINE
53
KAGERA
6
PS1701064 ROCKEN HILL
58
SHINYANGA
7
PS0202083 TUSIIME
168
DAR ES SALAAM
8
PS0702252 IMANI
29
KILIMANJARO
9
PS1701062 PALIKAS
19
SHINYANGA
10
  1. WATAHINIWA WALIOPATA ALAMA ZA JUU KATIKA MASOMO

Wapo watahiniwa walioweza kufaulu kwa kupata alama 50/50 katika baadhi ya masomo ambapo English Language walikuwa 7,600, Kiswahili 32 na Hisabati 34. Ingawa somo la Hisabati lina ufaulu wa chini zaidi kuliko masomo yote, watahiniwa 34 wamepata alama 50/50 katika somo hilo ambapo kati yao Wasichana ni 08 na Wavualana ni 26 kama ilivyo katika majedwali yafuatayo:

Orodha ya Wasichana waliopata alama 50/50 katika somo la Hisabati.

S/No
NAMBA YA MTAIHINIWA
JINA LA MTAHINIWA
JINA LA SHULE
MKOA
PS0203012-166 RACHEL IBRAHIMU KIUNSI KIMARA-'B' DAR ES SALAAM
PS0203077-020 MARIAM WILSON CHACHA PARADIGMS DAR ES SALAAM
PS0401041-023 DIANA PETER NJAU ST. CHARLES IRINGA
PS0501188-049 SOFIA GIDION NGERAGEZA ST. SEVERINE KAGERA
PS0904095-021 ANNABHOKE WAMBURA MAGORI TWIBHOKI MARA
PS0904095-022 ATUGONZA NEWTON KAMZOLA TWIBHOKI MARA
PS0904095-023 CATHERINE MOKORO MAGORI TWIBHOKI MARA
PS1701035-041 EDINA NGASSA SHABU KWEMA SHINYANGA
Orodha ya Wavulana waliopata alama 50/50 katika somo la Hisabati

S/No
NAMBA YA MTAHINIWA
JINA LA MTAHINIWA
JINA LA SHULE
MKOA
PS0202109-010 OMEGA AMOS LUGATA SABISA DAR ES SALAAM
PS0203058-021 JOHN REGINALD BUGERAHA MOUNTEVEREST DAR ES SALAAM
PS0401043-026 MANSOOR MOHAMED MALAMBO ST. DOMINICSAVIO IRINGA
PS0501188-007 ELIAH DANIEL MAKAMBA ST. SEVERINE KAGERA
PS0501188-013 GUSTAVIUS MWOMBEKI BAGAYA ST. SEVERINE KAGERA
PS0501188-017 MACHUMU NELSON SAMSON ST. SEVERINE KAGERA
PS0501188-018 MAPATO MAARIFA MAGESA ST. SEVERINE KAGERA
PS0501188-022 OBED LUCAS SAMWEL ST. SEVERINE KAGERA
PS0501188-023 OCTAVIUS IJUMBA MTAYOBA ST. SEVERINE KAGERA
PS0504092-004 DASTAN ADRIAN PIUS OMUKALIRO KAGERA
PS0504092-009 DICKSON NOVATH NDAULA OMUKALIRO KAGERA
PS0504092-015 MALICK AHMAD KUDABA OMUKALIRO KAGERA
PS0504092-016 MATHIAS GODFREY LUGALABAMU OMUKALIRO KAGERA
PS0504092-017 MICHAEL JONAS MICHAEL OMUKALIRO KAGERA
PS0504113-021 ROBERT INNOCENT NOEL TEGEMEO KAGERA
PS0702202-029 JUNIOR JOHNSON LOSARU SCOLASTICA KILIMANJARO
PS0702202-042 SAMSON HEAVENLIGHT NKYA SCOLASTICA KILIMANJARO
PS0904095-007 JAMES JOEL NYAROBI TWIBHOKI MARA
PS0904095-017 ROLLY GEDI MABURA TWIBHOKI MARA
PS0908004-020 EMMANUEL BENARD SARUNGI BUHEMBA MARA
PS1101170-004 HAJI ADAM NJALAMOTO ST. MARY'S MOROGORO
PS1104004-004 ABDULKARIM MIRAJI SAIDI UHURU MOROGORO
PS1701035-017 KISHIMBA MASUNGA SHIMBA KWEMA SHINYANGA
PS1703005-032 JACKSON PHANUEL MANGAIDA BUGARAMA SHINYANGA
PS2401020-013 MASANJA HEZIRON KABASA IHULIKE GEITA
PS2405080-028 NTOBI PAULO SUMBUKA KASANDALALA GEITA


  1. MPANGILIO WA MIKOA NA WILAYA KIUFAULU

  1. Mikoa Kumi iliyoongoza Kitaifa ni 

MKOA
IDADI
WALIOFAULU
(A-C)
ASILIMIA
NAFASI
DAR ES SALAAM
59,576
46,434
77.94
1
KILIMANJARO
37,918
26,192
69.08
2
MWANZA
53,596
37,017
69.07
3
IRINGA
21,363
14,650
68.58
4
ARUSHA
34,348
23,250
67.69
5
TANGA
39,066
26,261
67.22
6
NJOMBE
17,115
11,389
66.54
7
KAGERA
37,306
24,501
65.68
8
GEITA
27,854
17,560
63.04
9
MTWARA
25,015
15,608
62.39
10



  1. Wilaya Kumi zilizoongoza Kitaifa ni 

WILAYA
IDADI
WALIOFAULU (A-C)
ASILIMIA NAFASI
MPANDA MJI (KATAVI)
1,345
1,207
89.74
1
BIHARAMULO (KAGERA)
2,680
2,389
89.14
2
MOSHI(M) (KILIMANJARO)
3,565
3,145
88.22
3
KIBAHA DC (PWANI)
1,532
1,350
88.12
4
 ARUSHA (M) (ARUSHA)
9,097
7,919
87.05
5
KINONDONI(M) (DAR ES SALAAM)
11,110
9,533
85.81
6
KOROGWE VIJIJINI (TANGA)
4,868
4,118
84.59
7
ILALA(M) (DAR ES SALAAM)
12,091
10,038
83.02
8
IRINGA(M) (IRINGA)
3,250
2,681
82.49
9
MJI MAKAMBAKO (NJOMBE)
2,179
1,785
81.92
10



Maoni 2

Bila jina alisema ...

hongera kwa shule zote zilizotoka katika mikoa mipya

Nsolo S. Stephen alisema ...

Nawapongeza wanafunzi wote na shule zote walio/zilizoingia katika 10 Bora.