WAZIRI NYALANDU AVUNJA UKIMYA,ATOA KAULI NZITO JUU YA MAGAZETI,ATANGAZA KUMUUNGA MKONO WAZIRI MEMBE KWENYE HARAKATI ZA URAIS 2015 SOMA HAPA
picha ya pamoja kati ya Waziri Berdadi Membe kushoto pamoja na Rafiki yake Waziri Nyalandu.picha na Maktaba
Na Karoli Vinsent
BAADA ya kuandikwa sana kwenye
Vyombo mbalimbali vya Habari nchini,Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro
Nyalandu,ameibuka na kusema yote mabaya nayozungumziwa anamwachia mungu,kwani
wananchi wanamfuhamu kwa kazi nzuri anayofanya.
Kauli hiyo ametoa Usiku wa kuamkia leo Jijini Dar Es Salaam kwenye Hoteli
ya Kimataifa ya Hyatt Regency zamani ilikuwa inajulikana kama Kempiksi Hoteli,wakati
alipokuwa anafanyiwa Mahojiano na Mwandishi wa Mtandao huu,ambapo mwandishi wa
Mtandao huu alipotaka kufahamu ukweli unaoandikwa kwenye Magazeti mbalimbali
kuhusu yeye,ndipo waziri Nyalandu alisema anamwachia wananchi kwani
kinachaondikwa hakina ukweli wowote.
“Sikiliza mwandishi nimeandikwa sana vibaya na Magazeti tena wengine
wakinitaja kabisa kwamba mimi ni Jangili kama vile wanaushahidi ,baada ya
kuniona niko kimya wengine wakasema mimi ni Jasus wa CIA,ambaye nimepandikizwa
kwenye utawala huu mimi namwachia mungu tu kwani habari wanazoandika ni za
uongo hazina ukweli kabisa”alisema Nyalandu.
Nyalandu,aliyataja magazeti ambayo yanamwandika Vibaya , magazeti hayo
ni Jamhuri gazeti,Fahamu,Dira Mtanzania,Raia Mwema,magazeti hayo ambayo
yanatoka malamoja kwa Wiki.mwandishi wa Mtandao huu alipomuuliza kwanini
asiyachukulia Hatua kile wanachoakiandika kama ni cha Ukweli au la?
Nyalandu,alisema kwasasa hawezi kuyachukulia
hatua yeye anachofanya ni kuongeza ujuzi wa Ufanyaji kazi kwenye Wizara hiyo,na
wanaotaka kuendelea kumwandika vibaya wamwandike tu kwani wananchi wanaujua
mchango wake kwenye Wizara hiyo.
Kuhusu ukweli wa Taarifa ya kwamba
ni Jasus wa CIA
Waziri Nyalandu alisema hakuna hata
ukweli wowote kwamba yeye ni Jasus kwani ,hata hafamiani na hao majajus na kwanza
ni hivo ni vichekesho.
“Hivi kweli leo Naungana na Mh
Ridhiwani Kikwete kwamba waandishi wengi wa Nchi hii ni Makanjanja kwamba
hakuna ukweli wowote kwanza hawajuai wanavyoandika hivyo wanamwaibisha Rais
wetu wa Nchi kwani sisi tunavyochaguliwa tunakuwa tumefuzu sehemu zote na
tunakuwa hatuna Kashfa yeyote ndio maana Rais anatuamini”alisema Nyalandu.
Kuhusu kuhusika kumpigia Kampeni
Waziri Membe kwenye nafasi ya urais 2015 kwa madai ya kuadiwa kupewa Uwaziri
Mkuu.
Waziri Nyalandu ambaye ni Waziri Kijana
alizidi kusema taarifa hizo ni za ukweli,kwani Waziri Membe ni Rafiki yake
lazima atakuwa Rais 2015.
“Ndio mwandishi lazima nimpigie
Kampeni membe anafaa kuwa Rais na mwakani lazima aingie ikuru,na hapa
ninavyongea na wewe nikimaliza hapa kuongea na wewe naenda kuongea nae waziri
membe nakuhakishia lazima awe Rais 2015,kwani anasifa zote kwani wewe mwandishi
haoni sifa alizokuwa nazo?unamfananisha na wengine hao”alizidi kusema Nyalandu.
Kuhusu Waziri Nyalandu na Waziri
kivuli wa Wizara hiyo Mchungaji Piter Msigwa kuipigia chapuo kampuni ya
Uwindaji ya Windrose Safari(WWS) inayomilikiwa na wamarekani huku haina Sifa.
Waziri huyo ambaye alionekana kujibu
maswali kwa Hasira alisema Wizara yake haifanyi kazi kimajungu.
“Hizo taarifa zinaandikwa sana
kwenye Magazeti hazina ukweli wowote.kwanza mpaka unapewa kibali kwenye Kampuni
ya Uwindaji lazima uwe na Vigezo vyote kampuni hii inayo ndio maana tumeipa
nafasi hiyo sasa hao wanaolalamika huko kwenye Magazeti fahamu kwamba hawana
sifa hata kama kampuni yao ni ya Mzawa”alisidi kusema nyalandu.
Kuhusu DVD aliyoitoa Waziri Kivuli
wa Wizara hiyo mchungaji Piter Msigwa.
Nyalandu alisema taarifa hizo
amezipata na ameunda tume kuichunguza huo mkanda na kujua kwamba taarifa hizo
ni za kweli,.
“Nimeunda tume kuchunguza ukweli wa
huo mkanda na nimewapa wiki mbili na waje na majibu ya kulidhisha ili tubaini
ukweli wa ushahidi huo anausema msigwa na kwamba ni ukweli au la basi hatua
zichukuliwe “alisema Nyalandu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni