ZIFAHAMU SABABU NNE,ZITAKAZOMFANYA MSAKA URAIS LOWASSA KUTOINGIA IKURU,SOMA HAPA UJUE SABABU HIZO
Pichani ni Waziri Mkuu Aliyejiuzulu Edward Lowassa picha na Maktaba |
KUFUATIA minong’ono
ya Hapa na Pale kwamba ndugu Edward Lowasa kuwa amedhamiria kwenda Ikulu hata
kwa Kukipasua Chama chake,Kwa Mtazamo wangu na wa watu walio wengi, Hizi Hapa
Changamoto zinazomkabili Waziri huyo mkuu kutimiza ndoto yake hiyo.
Kwanza UFISADI
Popote linapotajwa jina la Edward
Lowassa, wazo la kwanza inayokuja
kichwani kwa msikilizaji ni ufisadi uliotukuka kwamba kila Watanzania wanapoikumbuka Richmond, wanamkumbuka
Lowassa, kwamba kila leo Lowassa analipwa na Serikali Mabilioni kupitia UFISADI WA RICHMOND.
Ni vigumu
sana kumtenganisha LOWASSA na RICHMOND, LOWASSA ni RICHMOND na RICHMOND ndo
LOWASSA, hili halikwepeki, na Watanzania sio wepesi wa Kusahau kiasi hicho,
Upo
UFISADI mwingi uliofanywa na LOWASSA, katika wizara zote alizowahi kuzitumikia
na nafasi zote alizowahi kuongoza, kwa sasa itoshe tu kusema LOWASSA ni
KIELELEZO KIKUU CHA UFISADI WA TAIFA HILI.
Pili UTAJIRI
MKUBWA
Yawezekana
ni Kutokana na UFISADI wake anaoufanya, lakini ukweli ni Kwamba LOWASSA ni
tajiri ambaye hata hawezi kusema mali zak amezipataje pataje, pamoja na
kumiliki mali nyingi hapa Tanzania, nyingi kati ya hizo akitumia majina ya
watoto zake na Maswahiba zake, lakini LOWASSA ni Miongoni mwa Watanzania
wanaomiliki Mali nje ya Nchi,
Picha hii ni ya Ikuru ya Tanzania ambayo Msaka Urais Edward Lowassa anataka kwa udi na Uvumba kuingia mwakani 2015.
|
Unaweza Ukajiuliza Mtumishi huyu wa
Serikali wa miaka mingi aliwezaje Kumiliki NYUMBA TATU za kifahari NCHINI
UINGEREZA?, NYUMBA ZA MABILLIONI YA SHILINGI, alitoa wapi utajiri huo?.
Gazti la
RAIA MWEMA NOV.2010 lilitoa MOJA KATI YA PICHA YA MAJUMBA YA LOWASSA NCHINI
UINGERZA.
Leo
anazunguka kugawa pesa hizi chafu makanisani na misikitini, UTAJIRI HUU UNA
MASHAKA MAKUBWA.
3.
KUKATALIWA NA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE
Kila mmoja anaijua nafasi ya mwalimu
nyerere kwenye maisha ya siasa za Tanzania.
Mwalimu
Tangu zamani alionyesha kutokumkubali kabisa LOWASSA, na kwamba UTAJIRI WAKE,
UBINAFSI WAKE, UFISADI wake na dhuruma zake nyingi alizozifanya zilimpelekea
mwalimu kuwa hataki hata kumsikia akishika nafasi kubwa za uongozi kwenye Taifa
letu.
LOWASSA,
ndio mgombea pekee anayepigiwa UPATU na viongozi na wanachama wa CHADEMA na
vyama vingine vya UPINZANI, sababu kuu ya kumpigia UPATU huo ni kwamba, wanaamini
kuwa LOWASSA ndio mgombea pekee ambaye ni Dhaifu na mwenye Kashfa na UBADHILIFU
mkubwa kwa Taifa hili hivyo kuwarahishia njia ya kumuangusha na wao kushinda
dola. Ndio maana huwezi kusikia popote Dkt.Slaa ama MBOWE akimsema vibaya
LOWASSA.
4.KUTOELEWANA NA MAKADA WENZAKE NDANI YA
CHAMA CHA MAPINDUZI CCM.
Hii ni
miongoni mwa sababu zinatazomfanya Waziri huyo mkuu wa zamani kusikia safari ya
kwenda magogoni ni Ndoto ni kutokana na kutoelewana na Makada wenzake wa
CCM,ikiwemo Waziri wa uhusiano wa Afrika Mashariki Samweli Sitta,ambaye
ameonekana kutokubaliana na Lowassa ambaye alidiliki kusema kamwe hawezi
kumpigia kampeni Lowassa hata kusimama kwenye Jukwaa moja la kumnadi kutokana
kutokuwa na kutokuwa na Sifa.
Mbali na Sitta,mtu mwengine aliyeonekana
kutokubaliana na Lowassa ni Kiongozi wa Juu Umoja wa Vijana wa chama cha
Mapinduzi UVCCM Poul Makonda alionekana kutoelewana kabisa na Edward Lowassa
ambaye anaye katika mkutano wake na Waandishi wa Habari alisema kwamba Lowassa
hana sifa ya kuwa hata kiongozi katika Taifa hili hata sifa ya kuwa Amiri Jeshi
mkuu ndani mwa Taifa hili.
Hii ni baadhi ya Viongozi walioko
ndani ya chama cha mapinduzi wasiokubaliana na sera za Lowassa pamoja na
Matendo yake na kwa hali hii safari ya Lowassa kuingia Ukuru mwakani 2015
inazidi kuwa Ndoto.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni