BREAKING NEWSZ--DK SLAA AMLIPUA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA,ASEMA ANATUMIWA ILI AKIHUJUMU CHADEMA,SOMA HAPA ALIVYONGEA NA MWANDISHI WA MTANDAO HUU,MDA HUU
Picha ya Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dk Willibrod Slaa,picha na Maktaba
Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita baada, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
kusema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod
Slaa hawana sifa za kugombea tena uongozi wa chama hicho kwa kuwa wanabanwa na
katiba yao,
Naye ,katibu mkuu wa chama hicho,ameibuka na kusema wao watapuuza kile
anachokiita ni njama zinazotumika kukibomoa chama hicho,kwani utaratibu
aliotumia aukufuata kanuni yeyote katika maamuzi hayo.
Kauli hiyo imetolewa mda huu na Katibu Mkuu chama cha Maendeleo CHADEMA,
Dk Willibrod Slaa wakati alipokuwa na anafanyiwa mahojiano na Mwandishi wa
Mtandao huu,kutaka kujua kuhusu kauli ya chadema baada ya maamuzi ya Msajili wa
vyama vya kisiasa,ambapo alisema Msajili wa Vyama vya Siasa amefanya maamuzi
bila ya kuwasialina na chama hicho,na maamuzi ya kufanya hivyo ni ishara sasa
msajili anatumika kukipomoa chama hicho.
Dk Slaa,aliongoza sababu anayoisema
kwamba chama hicho imeondoa kipengele cha ukomo wa uongozi sio kweli,bali
katiba ya chadema inahitaji mapendekezo yote ya katiba yaanzia kwenye ngazi za
Mabaraza ya wilaya na kupanda hadi kwenye baraza za mikoa.
“Katiba ya chadema inahitaji maoendekezo
ya mabadiliko ya katiba yaanzia kwenye mabaraza ya wilaya na kupanda hadi
kwenye baraza ya mikoa ya chama pamoja na mabaraza yake yote yaani ya
Vijana,wazee pamoja na wanawake,na yakitoka mapendekezo hayo mpaka yanafika
kwenye mkutano mkuu na kuyatotelea maamuzi”alisema Dk Slaa
Mwandishi wa Mtandao huu alipomtaka
kutolea ufafanuzi kuhusu kipengele cha ukomo wa Uongozi kilichotolewa kwenye
Katiba ya chama hicho.
Dk,Slaa alisema kifungo hicho
kilitolewa kwaanzia viongozi wa chini na wala sio matakwa ya viongozi wa Juu.
“Kifungu hicho kiliondolewa kutoka chini kwani katiba ilipelekwa huko
chini kwenye mabaraza na mapendekezo yapelekwa chini na kukakubalika na hicho
kipengele kilikubalika huko chini na kufika makao makuu yaanza kujadiliwa na
sisi ndio tulivyofanya, kumbukeni mkutano mkuu sio kazi yake kutunga
katiba kazi yake kupisha yale ambayo vyombo vyake vimefanyiwa kazi”alisema Slaa
Katika hatua nyingine Dk Slaa aliwashangaa watu wanaojiita viongozi wa
chama hicho kwa kuanza kuwalalamikia viongozi wa chama,kwani wamekaa kimya
kipindi cha miaka kumi kuja kulalamika sahivi.
“Nashangaa hawo viongozi wanalalamika,sasa kwanini wasingelalamika huko
kwenye kamati za wilaya na kamati za mikoa huko ndio wangelalamika,nashangaa
leo wanalalamika baada ya miaka kumi kupita ndio wanaanza kulalamika.”
“Harafu kunaviongozi walimaliza uongozi katika vipindi viwiliviwili,kama
kipengele hicho kingekuwepo kama Mzee ndesambulo asingechaguliwa 2009,
mala ya tatu kutokana na marekebisho katiba kumruhusu pamoja mzee Katisiko
Mkoani Kigoma amechaguliwa kutokana na Katiba kumruhusu,wako viongozi wengi
ambao wapo kutokana Katiba kumruhusu”alisema Dk Slaa.
Vilevile Dk Slaa,aliwataka wanachama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
kupuuzia maelekezo kutoka kwa msajili kwani ushauri wake hakuzingatia katiba ya
Chadema na kuwataka kupuuzia kwani unalengo kukivuruga chama hicho.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni