Zinazobamba

haya ndiyo makosa ya tundulissu: mwanasheria wa zitto afunguka




Mwanasheria mkuu wa Chadema,Tundu Lissu. 


Dar es Salaam. Wakili wa kujitegemea na Diwani wa Kata ya Mabogini mkoani Kilimanjaro (Chadema), Albert Msando ameeleza kasoro nne za kisheria ambazo zimefanywa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu wakati wa kutoa hukumu kwa makosa yaliyofanywa na makada wa chama hicho, Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msando alisema Katiba ya Chadema inaeleza kuwa kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya kupewa mashtaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashtaka hayo kwa maandishi.
“Tunaomba Lissu aeleze kwa njia ileile aliyotumia kueleza umma wa Watanzania uamuzi wa Kamati Kuu, siku na tarehe ambayo Dk Kitila na Zitto walipewa mashtaka yao kwa maandishi na atoe nakala ya majibu yao kwa maandishi kama yapo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema,” alisema na kuongeza:
“Aeleze ni utaratibu gani ulitumika kuwajadili kwenye kikao cha Kamati Kuu, kufikia uamuzi na kuwapa adhabu ya kuwavua madaraka wakati hawajapewa mashtaka hayo kwa maandishi kama Katiba inavyosema, kisha Kamati Kuu kwenda kwenye vyombo vya habari na kueleza kuhusu uamuzi huo na kutoa siku 14 ili wajieleze.”
Alisema Lissu hatakiwi kutoa majibu ya jumla, bali kueleza utaratibu, sheria na utawala bora gani uliotumika kuchukua uamuzi huo dhidi ya Zitto na Dk Kitila. Alisema Lissu pia anatakiwa kueleza aina ya ushahidi alionao ambao ulitumika kuwahukumu.


Hakuna maoni