HATARI SANA,VIPANDE 700 VYA MENO YA TEMBO VYA KAMATWA WANAPOISHI WACHINA JIJINI DSM
Zaidi ya vipande 700 vya meno ya Tembo ambavyo vinakadiriwa kuwa ni zaidi ya tembo 200 kama wangekuwa hai vimekamatwa katika maeneo ya mikocheni jijini Dar Es Salaam ikiwa ni katika makazi ya raia wenye asili ya China.
ITV ilifika katika eneo hilo na kufanikiwa
kushuhidia shehena hiyo huku baadhi ya raia wa China wakiwa chini ya
ulinzi wa polisi ambapo mmoja ya Wachina hao amesema hahusiki na mzigo
huo na amekuja nchini kwa ajili ya mapumziko.
Akizungumza katika eneo la tukio waziri wa malisi
na utalii mh balozi hamis kagasheki amesema mapambo bado ynaendelea
japo wapo watu hasa wabunge wanaobeza jitihadaza hizo.
Katika hatua nyingine baadhi ya wakazi wa maeeno ya
Mikocheni mtaa wa faru wamesema wanachojua ni kuwa Wachina hao
wanafanya biashara ya kuuza ndimu na vitunguu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni