Zinazobamba

FIBERHOME YAUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KUBORESHA MAWASILIANO.

Na Mussa Augustine 

Hivi karibuni Waziri wa Mawasilano na Teknolojia ya Habari Angellah Kairuki alizindua awamu ya pili ya Mradi wa "Fiber mlangoni kwako"awamu ya pili unaotekelezwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL)ikiwa lengo ni kuongezea upatikanaji wa intaneti yenye kasi,bora na uhakika.

Aidha Kairuki alisema mradi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha uchumi wa kidigitali kwa kuwa intaneti ya kasi inawezesha wananchi kupata fursa za elimu,ajira, biashara,ubunifu na huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Hivyo wadau wa Sekta ya Teknolojia ambao ni Kampuni ya mawasiliano ya FiberHome kutoka Nchini China imeunga mkono juhudi za Serikali kwa kueendesha kongamano (workshop)nchini Tanzania lililofanyika jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kuitangaza teknolojia yao Duniani na barani Afrika (World Tour).

Ziara hiyo imelenga kuleta mapinduzi makubwa ya Teknolojia ya mawasiliano na akiliunde (AI) ambayo tayari imefanyika katika nchi za Morocco, Algeria,na Kenya,huku ikitarajiwa kuendelea nchini Ethiopia na Afrika Kusini.

Akizungumza katika kongamano hilo, Afisa Mkuu wa idara ya ufundi  Bw.Michael Wang ameeleza kuwa lengo kuu ni kutoa elimu na kuonyesha jinsi teknolojia ya mawasiliano inavyokua kwa kasi pamoja na matumizi ya akiliunde(AI).

Wang amebainisha kuwa mzunguko huo wa ziara umepokelewa kwa matokeo chanya barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mazungumzo na Serikali ya Algeria ya kufungua kiwanda cha utengenezaji wa Kebo za Fiber(kama vile ADSS na Drop Cables) pamoja na vifaa vyake (accessories).

Akitofautisha FiberHome na Makampuni mengine,mwakilishi huyo amesema kuwa FiberHome inajikita zaidi kwenye ubora wa bidhaa kwa kuwa wao wenyewe ndio wanaotengeneza fiber kuanzia hatua ya awali kabisa hadi kuwa kebo kamili inayoweza kuhimili na kupitisha mawasiliano ya waendeshaji (operators)tofauti kwa wakati mmoja.(Picha ikionesha Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Angellah Kairuki akizundua mradi wa Faiba Mlangini kwako hivi karibu jijini Dar es salaam.)

Halikadhalika Wang,amesisitiza kuwa wanazingatia mahitaji halisi ya wateja wao (tailor-made solutions) badala ya kuuza tu bidhaa bila kujali nahitaji ya wateja.

Kuhusu uwepo wao nchini Tanzania ,amefafanua kuwa kwa sasa FiberHome inapatikana kupitia mitandao yao ya kijamii,lakini ipo kwenye mchakato wa kufungua ofisi rasmi nchini Tanzania ndani ya miezi michache ijayo ili kusogeza huduma karibu zaidi na wateja.

Hata hivyo kongamano hilo lilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya mawasiliano nchini,ikiwemo wawakilishi kutoka Makampuni ya Mawasiliano ya Vodacom na Airtel,Wakandarasi wa Serikali,Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),

pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Mawasiliano ambao wameipongeza kampuni hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za kuleta teknolojia ya kisasa nchini Tanzania

No comments