Zinazobamba

VIJANA 128 KUTOKA VYUO VIKUU MBALIMBALI NCHINI WAJIUNGA ACT WAZALENDO,ADO ATOA NENO.

Na Mwandishi Wetu.

Katibu Mkuu wa Act Wazalendo Ado Shaibu amewataka vijana wa Vyuo vikuu ambao ni Wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanapigania haki,Demokrasia na uwajibikaji kwa Taifa 

Ametoa maelekezo hayo leo Juni 14,2026 wakati akizungumza na vijana wa Vyuo vikuu wapatao 128 ambao wamejiunga na chama hicho,nakusema kuwa vijana wanapaswa kuwahoji Viongozi wa Serikali ambao wanashindwa kutekeleza wajibu wao katika kuleta Maendeleo kwa Taifa.

"Mmejiunga na chama sahihi,naomba msiwe waoga kujitokeza kuwahoji Viongozi ambao wamekua wakitoa majibu mepesi kwa Wananchi pindi wanaposhindwa kutatua changamoto za Wananchi huku Mamlaka zikishindwa kuwawajibisha."amesema Katibu Mkuu huyo.

Aidha ameendelea kusema kuwa vijana hao wanapaswa kusambaza mbegu za fikra ya  ukombozi kwa Taifa,nakuhakikisha wanapigania misingi mitatu ambayo ni haki,maslahi ya umma na Demokrasia,pamoja na uwajibikaji ili kupata Demokrasia ya vitendo.
"Mnawajibu wa kutetea haki kwa makundi yote,hivyo natoa agizo la chama kwa Ngome ya Vijana Act Wazalendo kutaka mapinduzi makubwa ya siasa katika vyuo vikuu"amesisitiza Shaibu ambaye pia ni Mbunge wa Tunduru.

Awali Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Act Wazalendo Abdul Nondo ameonesha hali ya kusikitishwa kufuatia vijana waliokamatwa hivi karibuni na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kughushi nyaraka kwa lengo la kujipatia Mikopo ya elimu ya juu.
Nondo ameiomba Serikali kuwachia huru vijana hao kwani walifanyia hivyo kwa lengo la kujiendeleza kielimu kutokana na vigezo vilivyowekwa  kupata Mikopo ya elimu ya juu kutoka HELSB kuwa sio mizuri.






No comments