VIJANA MSITUMIKE KISIASA KUVURUGA AMANI YA TAIFA:KILIBA
Na Mussa Augustine.
Rai hiyo imetolewa leo Mei 2,2026 na Mwenyekiti wa Taasisi ya mama asemewe Taifa,Geofray Kiliba wakati akizungumza na waandishi habari Jijini Dar es salaam,nakubainisha kuwa vijana wengi wamekua wakitumiwa na wanasiasa hao kwa lengo la kuvuruga amani ya Taifa.
"Nawataka vijana wa vyuo na vyuo vikuu kuacha kutumika kisiasa kuleta mgawanyiko wa Taifa,naomba vijana wa Kitanzania kurudi kwenye msimamo wetu ambao tunao kilasiku kuhakikisha hatudanganwyi"amesema Kiliba
Nakuongeza kuwa"Tunatakiwa vijana kuwa mabalozi wazuri wa Taifa letu,tusidanganyike,tualinde amani yetu kwa wivu mkubwa".
Aidha amesema vijana wana kila sababu ya kuhakikisha kwa gharama yoyote waliyonayo kubeba agenda ya kuhubiri amani, nakwamba Taifa likiharibika waathirika wakubwa ni vijana wenyewe,hivyo wanapaswa kuwa makini na watu wanaopotisha taarifa za fursa za kiuchumi zinazotolewa na Serikali ya Dkt.Samia Sululu Hassan.
"Wale wanasiasa wanaohamasisha vijana kuingia kwenye vurugu wana maslahi yao binafsi,nyuma yao kuna siri nzito,hivyo vijana msikubali kutumika kwa maslahi ya watu fulani."
Aidha Mwenyekiti huyo ametangaza rasmi kuwa balozi mwema wa kusambaza uelewa mpana wa fursa za uchumi kwa vijana.
"Mimi kama balozi kazi yangu kubwa ni kubaini,kutafuta uelewa,nakusambaza uelewa huo wa fursa za kiuchumi kwa vijana."
Aidha amesema kuwa Wizara mpya ya vijana imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuinua vijana kiuchumi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo,Biashara,Michezo na Utamaduni.

No comments
Post a Comment