Zinazobamba

ACT WAZALENDO YAITAKA SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WALIOTAJWA KWENYE RIPOTI YA CAG.


Na Mwandishi Wetu.Dar es salaam.

Chama Cha Act Wazalendo kimeitaka Serikali kuwafikisha mahakamani wahusika wa ubadhilifu wa fedha za umma  waliotajwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
 
Hayo yesemwa leo April,19,2026 na Katibu Mkuu wa Chama hicho na Mbunge wa Tunduru Mh.Addo Shaibu wakati wa uchambuzi wa ripoti ya CAG uliyofanyika Makao makuu ya chama hicho Magomeni Jijini Dar es salaam.

Aidha amesema kuwa ripoti za CAG zimekua zikitolewa na kubainisha maeneo yalioyofanyiwa ubadhilifu lakini wahusika hawachukuliwi hatua kali ikiwemo kufikishwa mahakamani hali ambayo inachangia kuendelea kuwepo kwa upotevu mkubwa wa fedha za umma.
"Ripoti ya CAG ya mwaka wa fedha 2024/2025 imeonesha upotevu wa fedha kiasi cha shilingi tirioni 7,ukilinganisha na shilingi tirioni 2.5 kwa mwaka wa fedha 2023/2024,hali hii inaonesha ni jinsi gani tunavyoendeleza ubadhilifu mkubwa uliozidi kushika hatamu,hivyo Serikali ya CCM ichukue hatua ya kuwapeleka mahakamani wahusika wote waliotajwa" amesema Mh.Shaibu.

Nakuongeza kuwa" Wananchi watumie ripoti ya CAG kuwahoji,kuwaonya,na kuwazomea Viongozi wa Serikali ya CCM kutokana na kuongezeka kwa ubadhilifu wa fedha za umma bila hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahusika waliotajwa kwenye ripoti ya CAG.

Akizungumzia kuhusu deni la Taifa,Mh.Ado Shaibu amesema kuwa deni lililopo kwa sasa ni tirioni 110 sawa na ongezekao la shilingi tirioni 12.70, ambapo deni hilo limekua kubwa nakwamba litawakamua Watanzania mifukoni mwao.

"Hili deni la Taifa la shilingi tirioni 110 ukiligawa kwa idadi ya Watanzania kwa mujibu wa sensa ya hivi karibuni utabaini kila mtanzania atalipa kiasi cha shilingi milioni moja na laki nane(180,0000)hivyo hili deni ni mzigo mkubwa  kwa Watanzania"amesema.

Nae Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara Isihaka Mchinjita amesema kwamba Serikali inapaswa kuchukua hatua madhubuti ya kukabiliana na athari ya mafuta iliyojitokeza kutokana na vita ya mashariki ya kati na kufungwa kwa mlango wa kupitisha mafuta wa Hormuz nchini Irani.
Amesema kuwa hatua hizo ni pamoja na kubadilisha mfumo wa matumizi ya mafuta kwenye vyombo vya usafiri ikiwemo magari,bajaji na pikipiki ili kutumia gesi asilia inayozalishwa nchini humo,hatua ambayo itasaidia kupunguza matumizi makubwa ya mafuta nchini inapotokea dhalura ya upungufu wa nishati hiyo.

Halikadhalika kiongozi wa chama hicho Doroth Semu amesema kwamba ripoti ya CAG imebainisha kuwa Bohari ya Dawa Nchini(MSD)inaidai Serikali kiasi cha shilingi bilioni 47.11,hali ambayo inaifanya MSD kushindwa kutoa huduma ya Dawa kwa muda muafaka,hivyo Serikali inapaswa kulipa deni hilo haraka iwezekanavyo.



No comments