ZINGIZIWA ITAPATA MAENDELEO MAKUBWA:KANIKI
Mgombea Udiwani wa Kata ya Zingiziwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Selemani Kaniki,amekishukuru Chama hicho kwa kumpa ridhaa ya kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025,huku akiwahidi Wananchi kupata Maendeleo Makubwa.
Hayo ameyasema leo Augost 15, 2025, mara baada ya kupokea barua rasmi ya uteuzi, katika Ofisi za CCM Wilaya ya Ilala, Kaniki amesema uteuzi huo ni heshima kubwa kwake na kwa wakazi wa Zingiziwa ambao amewahakikishia utumishi uliotukuka.
“Nakishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kuniamini na kuniteua rasmi kuwa mgombea wa udiwani wa Kata ya Zingiziwa. Hii ni furaha kubwa na ndoto niliyoiombea kwa muda mrefu kwa ajili ya kuwatumikia Wanazingiziwa,” amesema Kaniki.
No comments
Post a Comment