Zinazobamba

KUNJE GOMBALE MWIRU KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUPITIA AAFP.

Kunje Gombale Mwiru(mwenye shati katikati) akipongezwa kwa kupitishwa kuwa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na mwandishi wetu.
Wajumbe wa Mkutano  Mkuu  wa Chama Cha Wakulima Tanzania ( AAFP) wamempitisha,Kunje Ngombale Mwiru kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,pamoja na  Chuma Juma Abdallah kuwa mgombea Mweza.
Hatua hiyo imekuja wakati wa ‎Mkutano huo uliofanyika leo Aprili 29,2025 Temeke Jijini Dar es Salaam,baada ya kufanya uchaguzi nakuweza kuwapata wagombea hao ambao watapeperusha bendera ya AAFP nchi nzima kunadi sera za chama na kuomba ridhaa kwa Wananchi kukichagua chama hicho kwenye uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.

 Hata hivyo Mkutano huo umeshindwa kumpata mgombea wa Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokana na kura zilizopigwa kutofikia idadi kikanuni na kikatiba,nakupangwa kufanyika baadae.
Kunje Gombale Mwiru(mwenye shati katikati) akipongezwa kwa kupitishwa kuwa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika Mkutano huo pia Wajumbe wa Mkutano huo wamempitisha Grace J.Sambayi kuwa Makamu Mwenyekiti Bara.
Aidha,Mwenyekiti Taifa AAFP,Said Sudi ambaye alikuwa mgombea wa Urais wa Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar ameshindwa kutangazwa kua mshindi katika kinyang'anyiro hicho kutokana na kupata kura za ndio 16 pekee, kati ya kura 92 ambazo zilipigwa na wajumbe wote huku kura zaidi ya 70 zilikua za hapana.
Mgombea urais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Said Sudi(aliesimama) akizungumza kupinga matokeo yaliyomfanya akose sifa kikanuni ya kupitishwa kuwa Mgombea wa nafasi hiyo.

Hata hivyo Said Sudi ambaye ni mgombea Urais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alipinga matokeo hayo huku akidai kuwa kuna baadhi ya viongozi wa Chama cha AAFP wanashirikiana na viongozi wa CCM kumhujumu ili kumdhoofisha kisiasa kwani ameonekana kuwa mwiba wa siasa kwa CCM huko Zanzibar.

Nae Kunje Gombale Mwiru aliechaguliwa kuwa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa AAFP kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho na kunadi sera za chama kwa Wananchi ili kuweza kupata ushindi katika uchaguzi mkuu.

"Mimi ni mwanasiasa makini,nimzoefu katika siasa za hapa nchini,naamini nitaenda kunadi sera za chama kwa Wananchi ili waweze kujua nini ambacho tunahitaji kuwatendea wananchi katika kuwaletea maendeleo" amesema Kuje kwa bashasha kubwa.


No comments