Zinazobamba

Wananchi Luhita walia na magugu katika Ziwa Burigi


Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC  Nah.Mussa Mandia akizungumza na wananchi wa Mwalo wa Luhita wakati Bodi hiyo ilipofanya ziara katika Mwalo huo hawapo pichani.

Bodi ya TASAC yaahidi kushirikiana namna ya kuondoa magugu

Na Mwandishi Wetu

Wananchi Kijiji cha Luhita  wanaotumia Ziwa la Burigi wameliomba Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kuangalia namna ya kutoa magugu katika Ziwa hilo kutokana na changamoto  wanazozipata wakati wa kusafiri na kuvua samaki na vyombo vya usafiri majini.

Wananchi hao wameyasema hayo wakati ziara Bodi ya TASAC wakati walipotembelea Mwalo wa Luhita katika Ziwa Burigi kuangalia usalama wa usafiri wa majini katika Ziwa hilo.Mwenyekiti wa Usimamizi wa Mazingira ya Fukwe Mwalo wa Luhita Nelson Atanas akizungumza kuhusiana changamoto ya magugu katika mwalo Luhita katika Ziwa Burigi.

Mwenyekiti wa Usimamizi wa  Mazingira ya Fukwe (BMU) Nelson Atanas amesema kuwa katika kufany safari katika ziwa hilo upande wa Luhita imekuwa changamoto kutokana njia wanaoitumia wamechonga ambapo  vyombo vya usafiri majini viwili haviwezi kupishana.

Amesema  ujio wa Bodi kwao ni fursa ya kuweza kupata msaada namna ya kutoa au kupunguza magugu katika mwalo huo na kurahisisha usafiri wa kwenda upande wa pili ambapo wananchi wote wanategemeana kwa biashara.Matukio katika picha ya Bodi ya TASAC  na viongozi wa Kijiji cha Luhita.

Kwa upande wao mwananchi wa kijiji wa Mwalo wa Luhita Leopord Baltazal amesema kuwa utafika wakati kutokana na magugu hayo kuongezeka watashindwa kufanya shughuli za uvuvi pamoja na kusafiri kwenda upande wa pili na kufanya maisha yao kuwa magumu.

Akitolea ufafanuzi wa changamoto hizo  Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC  Nah.Mussa Mandia amesema kuwa TASAC  wanachukua changamoto  katika kufanyia kazi ili kuhakikisha shughuli zao ziendelee kutokana  na kuwa na mchango kwa mapato na maisha yao kwa ujumla.Mkazi wa Luhita Leopord Baltazar akitoa maelezo  kwa Bodi ya TASAC Kuhusiana changamoto ya miundombinu katika mwalo wa Luhita katika ziwa Burigi.

Amesema katika kushughulika na magugu ni pamoja kuwa na gati na miundombinu mingine ya huduma katika mwalo wa Luhita.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Bodi katika Mwalo huo amemwagiza Mtendaji wa kijiji kuandika kwa maandishi mahitaji yanayohitajika na kupeleka kwa Afisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa Kagera.Wafanyakazi wa TASAC na Meneja wa Forodha Mkoa wa Kagera mwenye miwani.

Nahodha  Mandia amesema kuwa licha kuwa na changamoto  hizo usalama unahitajika kutokana na sheria ya kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya uokozi wakati wote.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan iko karibu na wananchi katika kutatua changamoto na mengi yamefanyika kwenye Bandari ,Mialo ya Uvuvi na usafirishaji wa abiria.






No comments