WASANII KUPIMA AFYA YA MOYO DESEMBA 21 ,2024.
Na Mussa Augustine.
Akizungumza leo Desemba 13,2024 na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Steve Mengele maarufu kama " Stive Nyerere" amesema kuwa kampeni hiyo inatoa fursa kwa wasanii wa filamu kupima afya zao na kuweza kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo Moyo.
Aidha Stive Nyerere amewasihi Watanzania kupima afya zao mara kwa mara ili kujua hali ya afya zao nakuweza kuishi kwa umakini zaidi katika maisha yao kwa kuzingatia ulaji unaofaa.
"Wasanii waache kuchezea suala la afya,wajitokeze kwa wingi kujisajili kwenye mamlaka zilizokasimiwa ikiwemo Bodi ya Filamu Nchini,pamoja Baraza la Sanaa Nchini( BASATA) kwa ajili ya kutambulika nakuweza kupata huduma ya kupima afya yao bila gharama yoyote" amesema Steve Nyerere.
Nakuongeza kuwa" sisi tupo sambamba na mama yetu Dr Samia Suluhu Hassan ambaye amekua akiwapelekea huduma za matibabu wananchi hadi kwenye maeneo yao,hivyo tunaendelea kuhamasisha wananchi wapende kupima afya zao mara kwa mara ili kunusuru nguvu kazi ya Taifa.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dr.Peter Kisenge amesema kwamba magonjwa ya yasiyo ya kuambukiza yamekua tishio kubwa ambapo yanachangia kwa asilimia 9 ya vifo Vyote vinavyotokea kwa mwaka hapa Nchini Tanzania.
" Nyinyi ni kioo cha jamii ,tuungane kwa pamoja katika kupaza sauti ili jamii iweze kubadilika na kuona suala la kupima afya na kuzingatia ulaji unaofaa ni jambo la msingi katika maisha yao ya Kila siku" amesema Dr.Kisenge.
Nae Katibu Mtendaji wa BASATA Dr.Kenmond Mapana amesema kwamba BASATA itaendelea kushirikiana vyema na wasanii ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi zao,hivyo wanapaswa pia kuzingatia hali ya kulinda afya zao.
"Tumejumuika pamoja leo, hii ni dhahiri kuwa tunaushirikiano mzuri sana,nawaomba muendelee kujiandikisha ili siku ya tarehe 21,Desemba,2024 tujitokeze kwa wingi pale Kawe kwa ajili ya kupima afya zetu hususani afya ya moyo," amesema Dr. Mapana.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni