Zinazobamba

MZURI AFRIKA YAFIKISHA TEKNOLOJIA YA MZURI PRO TIL HANANG MANYARA.

Kampuni ya Mzuri Afrika imewafikia wakulima katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na kuzitambulisha kampuni zake zenye teknolojia za kilimo ikiwemo mashine ya kulimia ya Mzuri Pro til na mbolea za kimimina za aGrami Afrika.

Akizungumza na wakulima hao Mkurugenzi Mtendaji wa Mzuri Afrika na aGrami Afrika Shaaban Mgonja, amesema wakulima wanapaswa kuthubutu kutumia teknolojia za kisasa za kilimo ikiwemo zana za kulimia ambapo teknolojia ya Mzuri pro til inaweza kuwa mkombozi wa tija ya mavuno.

Mgonja amesema kuwa kwasasa kampuni ya Mzuri Afrika inajukumu moja kubwa la kuisambaza elimu ya matumizi ya mashine ya kulimia ya Mzuri Pro til inayotumia teknolojia ya kisasa rafiki ya mazingira kuandaa shamba huku mkulima akipata nafuu ya matumizi ya nguvu kazi shambani, kupunguza gharama za uzalishaji na kupata uhakika wa idadi ya miche shambani.

'' Mzuri pro til ni teknolojia nzuri yenye kumpa uhakika mkulima kuvuna kwa tija hata katika kipindi kigumu cha uchache wa mvua, teknolojia hii inapunguza gharama za uzalishaji shambani kwasababu inafanya kazi kwa mfumo wa kompyuta unaomuwezesha operator kujua idadi ya mbegu inayoingia shambani, kiasi cha mbolea n.k kwahyo ni teknolojia rafiki kwa mkulima''alisema Mgonja.Pamoja na hilo Mgonja amesema mashine ya Mzuri pro til yenye ukubwa wa mita tatu ina uwezo wa kufanya kazi nne kwa mara moja kwenye heka saba ndani ya saa moja sawa na dakika 60 Mzuri pro til inaweza kulima, kulegeza udogo, kuweka mbolea, kuweka mbegu kwa pamoja.Mgonja amewatoa hofu wakulima na kuwasisitiza kujenga utamaduni wa kubadili mtazamo hasa katika zama za kilimo bora cha kisasa kinachokwenda sambamba na matumizi ya teknolojia za kisasa za kilimo na zana za kisasa za kilimo.

Kwa upande wake Mhandisi Godchance Sambu Mwezeshaji wa Mafunzo ya Teknolojia za zana za Kilimo kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine SUA amesema teknolojia hiyo inahitaji mkakati wa dhati kuifikisha kwa vijana waendesha mitambo ya zana za Kilimo kwasababu uwepo wa mashine ya Mzuri pro til nchini ni moja kati ya fursa za ajira.

''Ujio wa mashine hii ya Mzuri pro til ni fursa ya ajira kwa vijana wa kitanzania hatuna haja ya kutumia operators kutoka nje ya nchi kuendesha mashine hii, SUA sasa tunatoa kozi fupi kwa waendesha mitambo ya za zana za kilimo ikiwepo matumizi teknolojia ya Mzuri pro til,'' alibainisha Mhandisi Sambu.

Teknolojia za kisasa za kilimo zinatajwa kuchochea ukuaji wa kilimo biashara nchini,  kukuza kipato cha mkulima mmoja mmoja na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Teknolojia hizo za kilimo  ni pamoja na zana za kisasa za kulimia zinazorahisisha kazi ya kuandaa shamba kupanda, kuweka mbolea  na kupunguza gharama za uzalishaji, ambapo miongoni mwa zana za kisasa za kilimo ni mashine ya kulimia ya Mzuri Pro til ambapo baadhi ya wakulima waliopata nafasi ya kuelimishwa kuhusu mashine hiyo wanaiona nafasi ya Tanzania kuilisha dunia.

Mashine ya kulimia ya Mzuri Pro til yenye upana wa mita tatu inahudumia heka saba kwa saa kwa kulima, kulegeza udogo, kupanda na kuweka mbolea kwa wakati mmoja ambapo tayari baadhi ya vijana wa Tanzania wameanza kujifunza kuendesha mashine hii chuo kikuu SUA kwaajili ya kuwahudumia wakulima.




Hakuna maoni