13 WAKAMATWA KWA WIZI WA MIUNDOMBINU YA SGR NA TANESCO.
ACP Gallus Hyera
Na Mussa Augustine.
Jeshi la Polisi kikosi cha Reli kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limefanikiwa kuwakamata raia wapatao 13 kwa kosa la kuiba miundombinu ya Mradi wa treni ya Mwendokasi SGR,pamoja na Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO).
Raia hao kati yao ni Watanzania ,Wakenya na Wachina China13,ambapo wameiba chuma chakavu, nyaya za shaba , raw copper bars , flat bars, Coppers wire zipatazo tani 14 za nyaya za shaba zilizofungwa kwenye njia ya reli ya kisasa (SGR) katika maeneo mbalimbali .
Hayo yamesemwa leo Desemba 17, 2024 Jijini Dar es salaam na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Kamanda wa kikosi cha Polisi Reli Tanzania Gallus Hyera wakati akizungumza na Waandishi wa habar.
ACP Hyera amesema kwamba uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa miundombinu hiyo hukatwa na watu ambao awali waliajiriwa kuwa mafundi na vibarua wakati wa ujenzi huku baadhi yao ni wafanyabiashara wa chuma chakavu hivyo kupelekea kasi ya uharibifu wa miundombinu hiyo.
"Baadhi ya wanunuzi wameweka mawakala kutafuta na kuharibu miundombinu ya SGR na TANESCO katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha muda wote wanapata kwa wingi nyaya hizi za shaba"amesema ACP Hyera
Nakuongeza kuwa" katika oparesheni hiyo Novemba 28,2024 mchana maeneo ya Mdaula Chalinze walikamatwa watuhumiwa 5 wakiwa na waya wa shaba kilo.7 na mmoja kati ya hao ni fundi umeme kampuni ya YAP MERKEZI inayotekeleza ujenzi wa miundombinu ya SGR.
Pia huyo ndiye aliyekamatwa na nyaya za shaba maeneo mbalimbali na Novemba 30,2024 Maeneo ya Visiga Mlandizi kwenye kampuni ya The African light investment Ltd inayomilikiwa na raia wa kigeni kutoka China na Kenya zilikamatwa nyaya za shaba za uzito wa kilo 882.5
Aidha amesema kuwa amekamatwa Paul Joseph (28) Msukuma, Mfanyabiashara wa chuma chakavi ,Msambazaji na Wakala wa kutafuta na kuharibu miundombinu ya miradi ya Serikali.
Aidha ameongeza kuwa tukio lingine limefanyika Desemba 2,2024 maeneo ya Visiga Miwaleni Mlandizi ambapo ulifanyika upekuzi kwenye nyumba inayomilikiwa na wamiliki wanthe African light investment Ltd ambao ni raia wa China na Kenya hivyo watuhumiwa walikutwa na nyaya za shaba kilo 3787.9 na nyaya hizo zilitambuliwa kuwa zimetokana na uharibifu kwenye miradi ya SGR na TANESCO,watuhumiwa hao wamekutwa na jumla ya Kilo 4,570.4 za nyaya pamoja na raw copper bars 44 zenye uzito wa kilo 971.5.
Kwa mujibu wa ACP Hyera uchunguzi uliendelea huko Kisemvule Mkuranga ambapo Desemba 4 mwaka huu zilikamatwa nyaya za shaba kilo 608.6(TANESCO) Kilo 37.6(SGR) na flat bars zilizozalishwa na kuyeyushwa,nyaya za shaba kilo.5,517.4 kwenye kiwanda cha chuma chakavu cha Metal Chem Internationa Co.Ltd na watuhumiwa wawili wamekamatwa.
ACP Hyera ameendelea kufafanua kuwa Desemba 5 mwaka huu maeneo ya Mwenge Kinondoni zilikamatwa nyaya za Shaba( Copper ) kilo 65.5 toka kwa wanunuzi wa chuma chakavu na watuhumiwa 2 walikamatwa wakiwa na waya wa shaba kilo 6.5 wakiwa katika harakati za kuuza
"Desemba 13,2024 huko Kisemvule Mkuranga walikamatwa wamiliki wa kiwanda cha Balochistan Group of Industrial (BGI) kulikutwa na Copper waya kilo 61 copper bars piece 19.kilogram 141 toka kwenye gari lenye namba za usajili T.141 DQG aina ya fuso"amesema
Nakuongeza kuwa "upekuzi uliendelea kufanyika zilikamatwa tena nyaya za shaba kilo 67 na Angle bars piece 426 zenye jumla ya kilo 7728 ambazo ni zao la copper waya na shaba hiyo imejumuishwa toka kwenye miundombinu ya miradi ya SGR na TANESCO watuhumiwa wawili wamekamatwa .
Amesema kwamba jumla ya watuhumiwa 13 wamefikishwa mahakamani kati yao wanane wamepandishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kibaha kwa makosa ya uhujumu uchumi, pia wengine watano wakipandishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni kwa makosa ya uhujumu uchumi pia
Hata hivyo Jeshi hilo la Polisi kikosi cha reli limetoa onyo kali kwa yoyote anayejipanga kufanya uhalifu huo wa kukata nyaya za shaba kwenye miradi ya SGR na TANESCO na kusisitiza kuwa watasakwa kwa nguvu zote na kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
ACP Hyera ametoa rai kwa wananchi wote kuendelea kulinda miundombinu ya miradi yote ya Serikali na kufichua njama na vitendo vya uhalifu kwa wanunuzi wa vyuma chakavu kuacha mara moja kununua nyaya za shaba zinazotokana na uhalibifu wa miundombinu ya Serikali .
Hakuna maoni
Chapisha Maoni