Zinazobamba

WHI YAPATA TUZO YA HESHIMA KUTOKA AUHF

Na Mussa Augustine.

Watumishi Housing Investments (WHI) imetunukiwa tuzo ya heshima ya Nyumba za Gharama Nafuu zaidi Afrika iliyotolewa na Taasisi ya mikopo ya Nnyumba Afrika ( Africa Union for Housing Finance -AUHF inayotambuliwa na umoja wa Afrika (Africa Union)

Hayo yamesemwa leo Oktoba 23,2024  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments( WHI) Dkt.Fred Msemwa wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam

Aidha Dkt Msemwa amesema kuwa tuzo hiyo  imetolewa katika mkutano mkuu wa AUHF Mwaka 2024 uliyofanyika Zanzibar hivi karibuni.

"Tuzo hii ya heshima inatambua jukumu la WHI katika kuwezesha wamiliki wa nyumba kwa watu wa kipato cha chini na kati Nchini Tanzania na juhudi zilizofanywa na (WHI) katika kuleta suluhisho la njia nafuu za malipo ya nyumba ikiwemo malipo endelevu yanayolipwa kipindi cha ujenzi bila riba pamoja na utaratibu wa mpangaji mnunuzi ambavyo vilitajwa kama sababu kuu za ushindi huu" amesema Dkt Msemwa

Aidha ameendelea kufafanua kuwa njia hizo zimeleta unafuu mkubwa kwa watu wanaotamani kumiliki nyumba,nakusisitiza kuwa nyumba za WHI zinauzwa kwa bei nafuu kwa kati ya asilimia 10 hadi 30 ikilinganishwa na nyumba kama hizo kwenye soko,huku bei ya kununua ikianzia shilingi milioni 38.

"Bei hizi pamoja na njia nafuu za malipo zimewasaidia watanzania wengi kufikia ndoto zao za kumiliki nyumba,hivyo tuzo hii pia inasherehekea kipindi maalumu kwa WHI kwani inatimiza miaka 10 ya ubunifu na uongozi katika sekta ya makazi" amesema Dkt Msemwa.
Nakuongeza kuwa" WHI inakuwa taasisi ya kwanza nchini Tanzania na Afrika Mashariki kupokea tuzo hii ya heshima,WHI iliibuka kinara kutoka kwa taasisi mbalimbali zinazohusiana na sekta ya makazi kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika.

Amesema kuwa ushindi wa WHI umetokana na utekelezaji wake wa kipekee katika kubuni na kutekeleza miradi ya nyumba yenye gharama nafuu zaidi na hivyo kuleta unafuu kwa wanunuzi ikiwalenga watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

Amesema kuwa AUHF ni shirika linalounganisha wadau wa makazi barani Afrika kwa zaidi ya miaka 40 ,l
nakwamba linawezesha washirika wake kuendeleza ufumbuzi zaidi wa makazi ya bei nafuu,hivyo juhudi za WHI kupunguza gharama za makazi nakutoa njia mbadala za malipo ilionekana kama hatua kubwa kuelekea kufikia maono hayo.



 

Hakuna maoni