Zinazobamba

Shule ya Awali na Msingi ya St. Mathew's ya Mkuranga Mkoani Pwani imeanza kufundisha lugha ya Kifaransa

Na Yasmine Protace,Mkuranga

SHULE ya awali na msingi ya st. Mathew's s iliyopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani,imeanza kufundisha lugha ya kifaransa kwa wanafunzi wake.

Hayo yalisemwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo,James Yona katika mahafari ya darasa la awali na darasa la Saba ya shule hiyo.

Yona anasema kuwa awali wanafunzi hao,walikuwa wakifundishwa lugha ya kiswahili, kiingereza, kichina na sasa wameongeza lugha ingine ya kifaransa.

" Wanafunzi kuanzia elimu ya awali hadi ya msingi wanafundishwa lugha ya kiswahili,kiingereza,kichina na kifaransa," anasema.

Anaongeza kuwa shule yao,imejiwekea  dira ambayo dira hiyo imechangia kuwapo na maendeleo makubwa katika ufaulu wa wanafunzi wao.

Anasema dira yao imesimamia Mambo makuu matatu ambayo ni malezi,elimu na usalama.

Anasema katika  malezi wanawafundisha watoto nidhamu ambayo inakuwa mkombozi katika maisha yao.

Anasema upande wa elimu,wanawafundisha watoto elimu ya darasani na nje ya darasa.

Anasema elimu nje ya darasa wanafunzi wanafundishwa,kulima mbogamboga kufua, ujasiliamali wa kupika keki, upambaji,kutengeneza sabuni za chooni, sabuni za kufulia,kutengeneza viungo vya chai,kucheza mziki.

"Elimu hiyo haiishii kwa watoto wa shule ya msingi Inaendelezwa mpaka shule zao za Sekondari ambapo wanafunzi ufundishwa kutengeneza nembo za bidhaazao ikiwamo kuwafundisha utafutaji wa masoko na kutunza mitaji," anasema.

Anaongeza kuwa,shule yao inasimamia usalama wa watoto kuanzia kuingia shule,kupanda gari la shule mpaka kufikishwa nyumbani.

Anaongeza kuwa shule yao inajali usalama wa watoto ambapo kuna CCVT zimefungwa ili kuongeza usalama zaidi.

Akizungumzia hali ya ufaulu katika matokeo ya darasa la Saba anasema kuwa katika mitihani ya miaka sita iliyopita ufaulu ulikuwa alama A na kuingia katika nafasi za shule 10 bora.

Mwalimu Yohana aliwaomba wazazi ambao watoto wao wanahitimu elimu ya awali na msingi wawarudishe katika shule hizo ili waendelee kunufaika na elimu inayotolewa katika shule hiyo kwa upande wa sekondari.

Mwenyekiti wa shule hiyo Askofu Froliani Katunzi kutoka kanisa la EAGT CITY CENTER anasema kuwa, Mambo mazuri yopo katika shule hiyo hivyo,wazazi na walezi wanatakiwa kuwarudisha watoto hao katika shule za Sekondari za Taasisi ya MHL.

" Mmeona wazazi na walezi watoto wa awali na msingi jinsi wanavyojiami I katikakujieleza,mmeona wanavyojua kuzungumza lugha zaidi ya tatu,wanajua masuala la ujasiliamali,hivyo wanapomaliza elimu ya awali warudi hapa wasome darasa la kwanza na wanapomaliza darasa la Saba warudi wasome kidato cha kwanza katika shule za Taasisi ya MHL," anasema.

Anaongeza kuwa kuwarudisha watoto katika shule hizo ni kuwasaidia kuendeleza vipaji vyao.

Anasema shule hiyo imewafu disha watoto ujasiliamali ambapo mtoto anapomaliza elimu yake anauwezo wa kujiajili na kuacha kuwa tegemezi.

" Wapo watoto hawajui ujasiliamali,wanamaliza mpaka vyuo vikuu,wanasubili ajira,lakini watoto wanaosoma katika shule zataasisi yaMHL wao wanajua ujasiliamali na wanapomaliza shule wanachochote cha kufanya na sio kukaa vijiweni

Pia Askofu huyo aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tano,ambapo milioni mbili zitalipiwa ada kwa wanafunzi wawili ambao wameonyesha uwezo mkubwa wa kuielezea shule yao huku shilingi laki tano imetolewa kwa mwanafunzi aliyemaliza hapo kidato cha sita na kutengeneza bendela I inayoelezea historia ya shule hiyo.

Peter Mtembei Mtendaji wa Taasisi ya MHL,anasema kuwa wanashule nane,ambapo tano ni Sekondari na tatu ni shule za awali na msingi.

Anazitaja shule hizo za Sekondari  kuwa ni st. Mathew's,ujenzii na Victori zilizopo Mkuranga mkoani Pwani,pia Image Vosa iliyopo Ilula mkoani Iringa na st. Mark's iliyopo Mbagala Jijini Dar es Salaam.

Anazitaja kuwa shule za awali na msingi kuwa ni st.mathew's ,ujenzi na Mark's zote zikiwa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Anasema shule zao kauli mbiu ni elimu,malezi na usalama.

Anasema kauli mbiu hizo zimezaa matunda  kwa wanafunzi wote walipitia katika shule.

Pia Peter aliomba mhasibu wa shule hiyo ya St.Mathew's kumpatia pesa ya kununua bodaboda mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita katika shule hiyo na kutengeneza bendera iliyoo yesha historia ya shule hiyo.

Mgeni rasim katika mahari hayo Nancy  Philipo Mutalemwa anasema kuwa,watoto watumie teknolojia kwa manufaa ya baadae na sio kutumia teknolojia kwa mambo yasiyofaa.

Nancy ambaye ni  katibu wa Taasisi ya nasimama na mama Tanzania,pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama Cha mapinduzi mkoa wa Pwani anasema kuwa,dunia ya Sasa imebadilika hasa kwa maisha ya watoto.

Anasema hali ya sasa ya dunia sio nzuri hivyo watoto wanatakiwa waandaliwe vizuri .

Anasema sio rahisi sana kuhakikisha watoto wanaishi vipi bira ya kuwa na uangalizi.

Shule za MHL zimeliona hilo  na kuwaandaa watoto kwa kumuamini mungu iluu ui aweze kwenda kufanikiwa kimaisha.

Anasema shule za MHL zinamwandaa mtoto ili awe na ujasili na uwezo kufanikiwa katika maisha yake.

Anasema mtoto akipatiwa elimu bira malezi hawezi kuwa na nidhamu.

Hakuna maoni