Zinazobamba

KITABU CHA "KURUDI KWA YESU" CHA ZINDULIWA


                    Askofu Aurelian Ngonyani

Na Mussa Augustine 

Askofu wa Kanisa la  The Truth Ministries ,Askofu Aurelian Ngonyani amezindua kitabu na Mfumo wa Kuuza kitabu hicho Mtandaoni kwa ajili ya kuhakikisha Watanazania wenye hali ya Kawaida ya Misha wanakipata kwa urahisi.

Kitabu hicho ambacho kimepewa jina la "Kurudi kwa Yesu" kitauzwa kwa shilingi elfu 5 pekee kwa njia ya Mtandao katika mifumo ya sauti( audio) na nakala Tete( pdf)

Akizungumza leo Agost 21,2024 na Waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi wa kitabu hicho  Askofu Ngonyani amesema kuwa kitabu hicho kimekusanya alama za nyakati kuelekea utimilifu wa unabii wa siku za Mwisho.

Amesema kwamba kitabu hicho amekiandika baada ya kufanya utafiti kwa muda wa miaka 20 katika Nchi ambazo matukio yaliyoandikwa katika biblia yaliyoekea ambapo baadhi ya Nchi hizo ni pamoj na Misri,Jordan,Uturuki,Israel,Ugiriki,Ufaransa,Ureno,na Italia kupitia Kampuni yake ya AUMARK.

Askofu Ngonyani ambaye pia ni Mwalimu wa Theolojia amesema kuwa amefamya utafiti wa usomaji mdogo wa kuhusu usomaji wa Vitabu Tanzania,nakubaini kuwa wasomaji wa Vitabu ni wachache sana,pia nilibaini wasomaji ni wachache kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu rahisi inayomwezesha Kila mtu kuwa msomaji wa Vitabu ,ili kujiongezea maarifaa". amesema Askofu Ngonyani

Nakuongeza kuwa," ili kukabiliana na tatizo hili niliazimia kutafuta mbinu rahisi za kimpa Kila mtu fursa ya kuwa msomaji wa Vitabu,hata kama ana uoni hafifu ,Hana muda wa kukaa mahali pamoja na kushika kitabu kukisoma".

Aidha amesisitiza kuwa kwa kutumia Wahandisi wa kitanzania ,amefanikiwa kuunda Mfumo rahisi wa uuzaji wa Vitabu unaotumia msaada wa akili Mnemba "Artificial Intelligence "(AI) ambapo mtumiaji wa simu janja( Smart Phone) anachopaswa kufanya ni kuhifadhi namba ya simu "0766111176 "nakutumia neno "Hellow au habari" kisha Mfumo utamkaribisha katika duka la Vitabu la kidigitali na utampeleka katika duka la "Ngonyani Store"

Aidha ameongeza kuwa kitabu hicho Cha "Kurudi kwa Yesu" kina kurasa 225,kimechakatwa na kuwekwa katika Mfumo wa sauti(audio) na nakala Tete( PDF ili kila mtu aweze kukipata kiganjani mwake kupitia Mfumo uliozinduliwa

"Maudhui ya kitabu hiki ni muhimu kwa Kila mtu kuyapata kwa kuwa yanafunua kweli za msingi kuhusu Maisha ya wanadamu ya sasa na baadae,kinajibu maswali wanayoumiza vichwa vya watu wengi kama vile,tukio la Kurudi Yesu,kipindi Cha Mpinga Kristo,Hatma ya Msikiti wa Al-aqsa na kujengwa kwa Hekalu la Tatu la Yerusalem,pamoja na kuweka Wazi matukio makuu ya Taifa la Israel." amesisitiza Askofu Ngonyani






Hakuna maoni