Staa wa Muziki wa Bongo Fleva Harmonize akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa Albamu yake ya "Muziki wa Samia" utakaofanyika Mei 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

STAA wa Muziki wa Kizazi  Kipya maarufu kama Bongo Fleva Harmonize anatarajia kuzindua Albamu yake ya Tano  May 25, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Harmonize amebainisha hayo leo Mei 20, 2024 akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema Albamu hiyo ameipa jina la ‘Muziki wa Samia’ akiwa na lengo kupongeza na kuunga mkono kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake.

Harmonize amesema album hiyo ni ya mwisho kwake na kusisitiza kuwa ameimba sana kuliko kawaida na ametengezeneza nyimbo 10 ambazo zote zinamlenga Rais Samia hivyo baada ya album hiyo atapumzika na kurefresh huku akiwa anaachia wimbo mmojammoja na sio album tena.

Harmo amesema siku ya uzinduzi huo itakuwa ni usiku wa mialiko na hakutakuwa na viingilio “Tumekusanya mazuri yote ambayo yanafanywa na Rais Samia na Serikali na kuyaweka kwenye kitabu kimoja cha kumbukumbu ambacho kitaishi milele kinachoitwa Muziki wa Samia,".