LICHA YA KUTUHUMIWA KUIBA VYETI RC MAKONDA AFANYA HIKI LEO,SOMA HAPO KUJUA
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika ziara ya
kukagua sehemu zilizokumbwa na mafuriko katika bonde la Mto Msimbazi,
baada ya mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali jijini Dar es
salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatahadharisha wakazi wa
bonde la mto msimbazi kuwa mvua zinazo nyesha zitaweza kuendelea kuleta
madhara kwa wakazi waishio mabondeni kutokana na uharibifu wa
miundombinu ya maji.
Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa bonde la mto
Msimbazi ambao walikusanyika kumsikiliza wakati alipokuwa akitembelea
maeneo hayo.
"kulingana na utabiri wa hali ya hewa mvua hizi zipo kati ya Milimita 30
hadi 35 na zikiendelea kuongezeka mpaka Milimita 50, maana yake hali
itakuwa ni mbaya zaidi hivyo waswahili husema kinga ni bora kuliko tiba
"Amesema Makonda
amesema kuwa wao kama Serikali chini ya Rais Magufuli wanategemea kupata
fedha kutoka benki ya Dunia ili kuweza kudhibiti na kutengeza mto
msimbazi ili kupunguza Madhara, kwani yanayo onekana leo ni tabia mbaya
za kwetu wenyewe wanadamu kuwa wakaidi pindi tunapoambiwa tusijenge
mabondeni tunakuwa wabishi, pia tunaambiwa tuhakikishe kuwa hatuharibu
zile kingo za maji sisi tunaharibu na kuziba kisha kujenga.
Post Comment