WAZIRI MWAKYEMBE ALIPUKA,AJIPANGA KUWAFUKUZA MAHAKIMU WENYE CHETI NA DIPLOMA,KISA NI HICHI HAPA,SOMA HAPO KUJUA

Waziri wa katiba na sheria Mh. Dkt Harrison
Mwakyembe amesema serikali itawafuta kazi mahakimu wote wa mahakama ya mwanzo
wenye elimu ya cheti na diploma ya sheria.
“Tunahitaji mahakimu wenye uwezo wa sheria ambao
wamehitimu shahada ya kwanza,hivyo serikali itawafuta kazi mahakimu wote wenye
elimu ya cheti na diploma”
Dkt mwakyembe ameyasema hayo leo jijini dar es
salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mswada wa sheria ya
msaada wa kisheria ambapo amewaomba wananchi na wadau wa sheria nchini kufanyia
mapitio mswada huo na kutoa maoni yao kwa kamati ya bunge ya katiba na sheria
wakati utakapowadia.
Dkt mwakyembe amesema bunge litaweka utaratibu
unaofaa kwa ajili ya kupokea maoni ya wadau wote watakaofika mbele ya kamati na
wale watakao wasilisha maoni yao kwa njia ya maandishi.
Aidha waziri mwakyembe ameelezea mswada huo ambao
umesomwa bungeni kwa mara ya kwanza tarehe 10 novemba utawatambua watoa huduma
za msaada wa kisheria na utakuwa ni ukombozi kwa jamii ya watanzania walio
wengi ambao hushindwa kumudu gharama za kuwalipa mawakili.