TUKIO KUBWA ALILOFANYA WAZIRI NCHEMBA LEO NDANI YA IDARA YA UHAMIAJI,RIPOTI HII HAPA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba, akizungumza na baadhi ya wananchi waliokuja kupata
huduma Makao Makuu ya Idaya ya Uhamiaji wakati wa ziara yake ya siku
moja aliyoifanya leo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Waziri Mwigulu akiwasili kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za makamishna wa Uhamiaji zinazojengwa Kijichi jijini Dar es Salaam kuzikagua. |
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Abbas Rovya (kushoto), akimpigia saluti Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) kabla ya kukagua
nyumba hizo za kisasa. Kulia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI),
Shaban Hamza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba (kulia), akiangalia nyaraka mbalimbali zinazochapishwa
katika kiwanda cha kuchapa nyaraka za Uhamiaji alipotembelea kiwanda
hicho kilichopo Kijichi jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni
Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji (ASP), Singwa Mokiwa na Kaimu Kamishna
Generali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Mwigulu mbali ya kutembelea
kiwanda hicho na mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa za makamishna wa
Uhamiaji pia alizungumza na wafanyakazi wa Uhamiaji makao makuu
Kurasini.
Waziri Mwigulu akipata maelezo zaidi ya uchapishaji kwenye kiwanda hicho.
Kaimu Kamishna Generali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Mwigulu.
Waziri Mwigulu akiangalia nyaraka mbalimbali kwenye
kiwanda hicho.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Lusungu Ngairo (katikati), akimueleza jambo Waziri Mwigulu wakati wa ziara hiyo.
SERIKALI
imesema itaboresha mitambo ya kuchapisha nyaraka ya Uhamiaji ili kupata nyaraka
zenye ubora wa kisasa.
Hayo
yamebainishwa Dar es Salaam leo mchana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba wakati alipotembelea Kiwanda cha kuchapisha Nyaraka cha
Uhamiaji kilichopo Kijichi Temeke jijini Dar es Salaam.
"Napenda
kuwapongeza wenzetu wa Uhamiaji kwa kuwa na kiwanda cha kuchapisha nyaraka zao
sisi kama serikali tutaongeza nguvu ndani ya taasisi hii ili kupata nyaraka
bora zaidi " amesema Nchemba.
Mwigulu
alisema nyaraka nyeti za serikali ni vizuri zichapwe na taasisi husika kama
wanavyofanya uhamiaji jambo litakalosaidia kutozagaa hovyo mitaani.
Kwa upande wakeKaimu Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Abbas Irovya
wakati akitoa taarifa ya kiutendaji ya idara hiyo kwa Waziri Nchemba, amesema changamoto ya uhaba wa wafanyakazi ni moja ya
sababu ya idara hiyo kushindwa kuwadhibiti.
Pamoja na kutokuwepo kwa mifumo ya kisasa na vyombo vya usafiri vya kutosha.
Hata hivyo, Irovya amesema uhamiaji imepokea maombi ya watu wanaotaka uraia 198 pia imekagua watu 1137000 katika mipaka mbalimbali nchini.
Kuhusu ukusanyaji mapato, amesema idara hiyo imevuka lengo la ukusanyaji mapato kwa asilimia 67 kutokana kwamba ilikuwa na lengo la kukusanya bilioni 108 kwa mwaka huu wa fedha na kwamba imekusanya zaidi ya bilioni 180
Waziri
Mwigulu aliongeza kuwa hivi sasa mpango wa serikali ni kutengeneza bidhaa zake
kupitia taasisi zake kama ilivyo kwa viatu ambapo wameelekeza vitengenezwe na
Magereza na kutumiwa na vyombo vyote vya ulinzi na usalama.
Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk.John Magufuli la kuzipa uwezo taasisi za serikali hasa majeshi kujiimarisha kwa kufanya kazi za viwanda zenyewe kama za utengenezaji wa madawati, uchapishaji wa nyaraka kama wanavyofanya Uhamiaji na nyingine nyingi
Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk.John Magufuli la kuzipa uwezo taasisi za serikali hasa majeshi kujiimarisha kwa kufanya kazi za viwanda zenyewe kama za utengenezaji wa madawati, uchapishaji wa nyaraka kama wanavyofanya Uhamiaji na nyingine nyingi