Gwajima afyatuka tena, amshauri Magufuli aihame CCM....Adai amenasa njama Mbaya
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye anafahamika kwa kutoa kauli ‘tata’, amefyatuka tena akimshauri Rais John Magufuli kuihama CCM endapo kile alichokiita ‘njama alizozibaini’ ndani ya chama hicho zitaletwa mezani.
Gwajima
ambaye amekiri kuwa katika kampeni alikuwa hamkubali Dk. Magufuli
kutokana na kutokuwa na imani na CCM, amesema amemkubali sana baada ya
kuanza kazi ya urais kutokana na hatua ambazo amekuwa akizichukua ndani
ya muda mfupi.
Akizungumza
katika ibada ya Jumapili kanisani kwake, Gwajima ameeleza kuwa amebaini
njama za baadhi ya wanachama wa CCM ambao ‘dili’ zao mbalimbali ikiwa
ni pamoja na ‘flow meter’ ya mafuta yaingiayo nchini na makontena
yaliyokamatwa yalikuwa yanawahusu, wameanza kampeni ya chinichini nchi
nzima kutaka Rais Magufuli asipewe uenyekiti wa chama hicho.
Amesema
kuwa watu hao wanazunguka nchi nzima kuwashawishi wanachama wa CCM
kuridhia hoja ya kutenga uenyekiti wa chama na urais, ili kumnyima
nafasi hiyo Rais Magufuli ambaye utendaji wake umewabana bila kujali ni
wa chama chake.
Hivyo,
amemshauri Rais Magufuli kuwa endapo itatokea hilo, akihame chama hicho
na kuendelea na kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni