ASKOFU MALASUSA ALIPASUA KANISA LA KKKT,KASHFA LUKUKI ZAMWANDAMA,SOMA HAPO KUJUA
SAKATA la tuhuma za uzinzi kati ya Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli (KKKT), dayosisi ya Mashariki na Pwani
(DMP), Dk. Alex Malasusa, linazidi kuchukua sura mpya, anaandika Mwandishi Maalum.
Mchungaji Leita Ngoy, anayedaiwa kuzini na Askofu Malasusa,
amegomea mwajiri wake kwenda likizo iliyolenga kumuweka mbali na mkuu wa
kanisa.
Taarifa ndani ya
dayosisi hiyo zinasema, katibu mkuu wa DMP, Godfrey Nkini, amenukuliwa
akimueleza Mchungaji Leita kuwa utendaji wa Askofu Malasusa wa kuhudumu ofisini
umezorota tangu kuibuka kwa tuhuma hizo. Akamtaka kwenda likizo ili kurejesha
amani ya kiongozi mkuu wa dayosisi.
Haya yameibuka
baada ya jitihada za kutaka wachungaji kumtetea Askofu wao kushindikana. Hoja
ya kutaka kanisa limfanyie maombi Askofu Malasusa iliwasilishwa kikaoni na
msaidizi wa Askofu.
“Baada ya mpango
huu kukwama, katibu mkuu wa dayosisi alimwita Mchungaji Leita ofisini mwake na
kumtaka achukue likizo ya muda mrefu ili asionekane machoni mwa waumini na
wageni wengine.
“Mchungaji Leita
alitoa masharti mawili: Kwanza, yuko tayari kuchukua likizo endapo katibu mkuu
atampa barua rasmi ikieleza sababu ya hatua hiyo na pili endapo mtuhumiwa
mwenzake, Askofu Malasusa, naye atapewa likizo.”
Amesema, “katibu
mkuu Nkini ameshindwa kutekeleza masharti hayo, jambo ambalo limesababisha
Mchungaji Leita kuendelea kubaki ofisini.”
Haya yanaibuka,
siku mbili baada ya Asime Modern Mwakilima, muumini wa dayosisi ya Mashariki na
Pwani akisema, anatafakari upya uumini wake katika kanisa hilo.
Alisema, “suala
la imani ni langu mwenyewe na Mungu. Lakini katika hili, naona mkuu wetu
amepoteza sifa ya kuhudumu. Badala ya kusimamia ukweli, kanisa limeamua
kukandamiza haki.”
Mchungaji mmoja
wa kike aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini ameutuhumu uongozi wa
dayosisi hiyo kukumbatia alichoita, “mfumo dume.”
Alisema, “hapa
kuna mfumo dume. Ndiyo unaotaka kutumika kumuonea huyu mama na kumlinda Askofu
aliyetuhumiwa naye. Haya ni makosa makubwa sana. Hata Bwana Yesu alipoletewa
mwanamke aliyefumaniwa akizini, alimwuliza yuko wapi mtuhumiwa mwenzako?”
Taarifa
zinasema, mkuu mpya wa KKKT, Askofu Fredrick Shoo amemuita Mchungaji Leita kwa
lengo la kujadiliana naye juu ya suala hilo; lakini amegoma hadi mahojiano hayo
yamshirikishe Askofu Malasusa.
“Hii inaonyesha
mchungaji huyu wa kike alivyonusa mbinu chafu za kutaka kutelekezwa na kanisa
ili kumuokoa Askofu Malasusa,” ameeleza mtoa taarifa ndani ya kanisa hilo.
MwanaHALISI Online ilipokea nakala ya waraka wa
kichungaji uliosambazwa kwa watu mbalimbali, ukiwataka waumini wa kanisa hilo
kuchukua hatua za haraka kuikoa dayosisi yao iliyotumbukia katika mgogoro wa
kuongozwa na anayemuita, “kiongozi aliyepungukiwa na uadilifu.”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni