WABUNGE WA CCM WALIGEUZA BUNGE KUWA SEHEMU YA MATUSI,SOMA HAPO KUJUA
KAULI ya ‘matusi’ iliyotolewa jana na Goodluck
Mlinga, Mbunge wa Ulanga Mashariki (CCM), imesababisha wabunge wanawake kutoka
vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutimuliwa nje, anaandika
Kelvin Mwaipungu.
Jana Mlinga alitoa kauli iliyotafsiriwa
na wabunge hao kwamba, ndani ya Ukawa ili wabunge hao wapate nafasi hizo lazima
‘wachojoe.’
“Mheshimiwa Spika, kuthibitisha hilo ili upate
ubunge ndani ya Kambi ya Upinzani lazima uitwe ‘baby’.
“Watu hawa wamefikia hatua ya kuwa na mahusiano ya
jinsia moja,” alisema Mlinga. Kauli hiyo imesababisha mtifuano leo na kupelekea
Job Ndugai, Spika wa Bunge kuwatoa nje wabunge hao.
Wabunge hao wanawake walianza kufanya fujo ndani ya
Ukumbi wa Bunge baada ya Mlinga kushindwa kuomba radhi kutokana na madai ya
kuporomosha matusi dhidi ya wabunge hao.
Kabla ya kutolewa nje, wabunge hao waliomba muongozo
kutoka kwa spika kutaka Mlinga afute kauli yake, spika hakuruhusu na hapo ndipo
fujo zilianza kuibuka.
Wabunge ha wametafsiri kitendo hicho kama
udhalilishaji ambapo wamepanga kuiandikia barua Ofisi ya Bunge ikiwa ni pamoja
na kutishia kujitoa katika Chama cha Umoja wa Wabunge Wanawake wa Bunge la
Tanzania.
Wameeleza kuwa, kukaa kimya kwa wabunge wanawake wa
CCM kunaonesha kuridhika na matusi waliyoporomoshewa hatua ambayo wameeleza
kutoifumbia macho.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni