Zinazobamba

AZANIA BENKI YARUDISHA Milioni 130 KWA WANANCHI,


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akishuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Godfrey Dimoso (kushoto) na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania William Kallaghe (kulia), wakitia saini mikataba ya kudhamini mbio za watoto za Azania Kids. Thamani ya udhamini huo ni shilingi milioni mia moja na therathini(130,000,000)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa kudhamini mbio za watoto za Azania Kids zinazotarajiwa fanyika Juni 5 mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Godfrey Dimoso  na Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki hiyo Mwanahiba Mohammed Mzee, wakisaini mkataba wa udhamini wa mbio za watoto  za Azania Kids


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Godfrey Dimoso (kushoto) na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania William Kallaghe (kulia), wakibadilishana mikataba ya kudhamini mbio za watoto za Azania Kids. mbio hizo zinashirikisha watoto chini ya umri wa miaka 16 na zinatarajiwa kufanyika juni 5 Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mara baada ya zoezi la kutia saini mikataba ya udhamini, Makonda amewapongeza Benki ya Azania kwa kuthamini mchezo wa Riadha na kuwahakikishia kuwa ofisi yake itatoa msaada utakaohitajika ili kufanikisha mbio hizo



Benki ya Azania imeamua kurudisha Milioni 130 kwa wananchi kwa staili ya aina yake baada ya kutumia fedha hizo kwa kufadhili mbio za watoto wadogo wenye umri chini ya miaka 16 zitakazojulikana kama Azania Kids.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw Godfrey Dimoso alisema Benki hiyo imedhamini mbio hizo ikiwa ni sehemu ya kurudisha kidogo walichopata kwa wananchi  kama wanavyofanya katika sekta zingine
Amesema ni utaratibu wa kawaida waliojiwekea kuhakikisha  benki inashiriki katika masuala ya kijamii ikiwamo sekta ya michezo
Akizungumzia sababu za kuvutiwa na wazo la kudhamini mbio za watoto, Bw. Dimoso alisema wamevutiwa sana na kitendo cha kujmjengea motto Tabia ya kupenda mchezo wa riadha ambao kwa muda mrefu bado haujaweza kutuletea medali.
Ameongeza kusema, haijawi kutokea kwa kampuni yoyote hapa nchini kudhamini mbio za watoto, lakini wao wanaona kuna umuhimu mkubwa wa kujenga utaratibu wa watoto kupenda mchezo wa riadha ili waje kuleta medali mbalimbali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki hiyo Mwanahiba Mohammed Mzee amesema wanataraji jumla ya watoto 2000 watashiriki katika mbio hizo za siku moja na kwamba wanataraji wakazi wa Dar Es Salaam watajitokeza na watoto wao kushiriki mbio hizo.

 “ Mbio hizi zitashirikisha watoto wengi tunataraji kuwa na Wazazi au walezi ambao watakuwa wanawasaidia watoto wao kukimbia…Zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wale washindi”Alisema
Mbio za Azania Kids zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mmnazi mmoja Juni 5, 2016 na kwamba wadhamini wngine wa mbio hizo wanatarajiwa kuwa New habari,Azam Media na Imaging.

Hakuna maoni