AKILI YA MBUNGE KUBENEA JIMBONI KWAKWE,MWILI WAKE BUNGENI,TIZAMA ALICHOFANYA KWA WANANCHI WAKE,SOMA HAPO KUJUA
Balozi wa Kuwait aliyevaa kanzu,
Jasem Alnajen akiwa amefungua maji ikiwa ni ishara ya kuzindua kisima cha maji
kilichojengwa kwa msaada wa nchi hiyo eneo la Golani, Kimara jijini Dar es
Salaam, jana kupunguza adha ya shida ya maji. Kushoto ni Mbunge wa Ubungo Saed
Kubenea na kulia ni Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota.
|
WANANCHI wa Golani, Kimara katika Jimbo la Ubungo,
jijini Dar es Salaam wamemshukuru Saed Kubenea, mbunge wa jimbo hilo kwa
kuwasaidia kupata kisima cha maji, anaripoti Regina Mkonde.
Wametoa shukurani hizo wakati
Jasem Alnajen, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania akikabidhi kisima cha maji kwa
Kubenea kwenye eneo hilo.
“Tulikuwa
na shida kubwa ya maji hapa, kwa hakika huu ni msaada mkubwa kwetu.
Tunamshukuru mbunge wetu kusaidia upatikanaji wa kisima hiki,” ameeleza
Beatrice Samweli, Mkazi wa Kimara.
Hata
hivyo, Kubenea amemuomba Balozi Alnajen kuwa mlezi wa eneo hilo sambamba na
kuendelea kutoa misaada mbalimbali jambo ambalo ameridhia.
Miongoni
mwa shughuli alizokubali serikali yake ya Kuwait kusaidia eneo hilo ni ujenzi
wa shule, zahanati, ukarabati wa barabara, kumalizia msikiti ikiwemo
uchimbaji wa visima vingine vitano.
Wakati
akipokea kisima hicho Kubenea alimshukuru balozi huyo na kuwaeleza wananchi hao
kwamba, jitihada hizo zimetokana na ahadi aliyotoa ya kuwapunguzia tatizo la
maji katika eneo hilo.
Amewataka
wananchi hao kuhifadhi kisima hicho ambacho kitakuwa mwanzo wa
visima vingine katika kampeni ya kumaliza tatizo la maji ambalo limekuwa kwa
muda mrefu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni