Zinazobamba

BILIONEA LUGUMI NI KIBURI,AWAKIMBIA WAANDISHI WA HABARI ALIOPANGA KUKUTANA NAO,AZIDI ICHEZEA SHARUBU SERIKALI YA MAGUFULI,





SAID Lugumi ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Lugumi Enterprises ambayo imengia mkataba tata wa zaidi bilioni 37 na Jeshi la Polisi nchini mmilikihuyo amezidionyesha umwamba wake baada ya kuwakimbia waandishi wa Habari ambao alipanga kukutana nao.Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo Jijini Dar es Salaam,ambapo Lugumi alitakiwa kuongea na waandishi wa habari katika ofisi yake majira ya saa sita mchana,ambapo waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti vya habari walijitokeza,

Mara baada ya mda huo wa kuanza mkutano kufika,Lugumi naye alikuwa hajafika,ndipo wanahabari wakasubili mpaka kufika saa saba mchana ndio akajitokeza msemaji wa Kampuni ya Lugumi aliyejitamburisha kwa jina Jumma Moshy Sabury  na kuwaambiana wanahabari Lugumi amepata safari ya ghafla.

“Jamani Lugumi hataweza kuja  kwenye mkutano huu,kwani amepata safari ya ghafla na ameenda  Dodoma kukutana na wabunge kuzungumza nao,”amesema Sabury.

Licha Sabury kusema haya,akatoa Tamko ambalo amedai limetoka kwa Lugumi,huku tamko hilo likiwa linatolea ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari.

Tamko hilo lenye kurasa mbili licha ya kukanusha kuwa mkataba wa lugumi kuwa ni wa halali pia Tamko hilo lilishindwa kuonyesha sababu ya Kampuni hiyo kushindwa kumaliza ufungaji   mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchi nzima huku akifunga mashine 14 tu,wakati amelipwa asilimia 99 ya malipo yote ambazo ni bilioni 34,
Jambo lilowafanya Waandishi wa Habari kumuliza msemaji huyo lakini alishindwa kutolea ufafanuzi.

 WANAHABARI WANENA.
Akizungumza kwa kujiamini Mmiliki wa blog ya Fullshangwe, John Bukuku amesema Lugumi anachezea akili za Watanzania 

Amesema kama kweli alikuwa na safari ya kwenda Dodoma kulikuwa na haja gani ya kuita mkutano na waandishi wa habari.
Kinachooneka hapo ni kwamba Lugumi ameamua makusudi kuwakimbia waandishi wa habari akijua wazi asingeweza kujibu maswali yao. 
."Yaani kama kuna siku Kampuni ya Lugumi Imechemsha basi ni leo, kuwakimbia wanahabari sio mwisho wa matatizo badala yake itazidi kuongeza tatizoa"Alisema Bukuku.
Naye Mmiliki wa Fatherkidevu blog amesema ameshangazwa kuona mmiliki wa Kampuni hiyo anatoa nakala kwa waandishi wa habari badala ya kuja kujibu hoja za msingi anazotuhumiwa.
Amesema wanahabari walitarajia angejitokeza kuja kupangua hoja mbalimbali ambazo zinachafua kampuni yake lakini imekuwa kinyume chake 
  UTATA WA KAMPUNI YA LUGUMI.
Katika mkataba huo, Kampuni ya Lugumi ililipwa kiasi Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha za makubaliano ya mkataba, lakini hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 pekee jijini Dar es Salaam ambavyo hata hivyo haijaainishwa maeneo vilipo,kwa mujibu wa taarifa mbali mbali zinasema kati ya mashine hizo 14 ni mbili tu zinazofanya kazi.

 Mkataba huo wa Polisi na Lugumi umezidi kuchukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kunyang’nywa hoja hiyo na badala yake kuhamishiwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Hatua hiyo inatokana na utata uliogubika mkataba huo ambao unawahusisha vigogo kadhaa wa Jeshi la Polisi pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, huku ikidaiwa kuwa huenda ikawa njia ya ‘kulindwa’.

Kutokana na hali hiyo, hadi kufikia Jumatatu saa 10 jioni, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly, alisema kuwa kamati yao haijapokea taarifa yoyote kuhusu Kampuni ya Lugumi, ambapo kamati hiyo ililitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha mkataba huo

Hakuna maoni