WABUNGE WA UKAWA DAR WACHACHAMAA,WAMGOMEA MKUU WA MKOA,SOMA HAPO KUJUA
Saed Kubenea, Mbunge wa jimbo la Ubungo
(kushoto) na Halima Mdee, Mbunge wa Jimbo la Kawe
WABUNGE wa vyama vinavyounda Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) jijini Dar es Salaam leo wamemgomea Meck Sadick,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kushiriki Kikao cha Kamati ya Ushauri (RCC) Mkoa
wa Dar es Salaam kwa madai ya kutotendewa haki, anaandika Happyness
Lidwino.
Wabunge hao waliandikiwa barua na Theresia Mmbando, Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwaarifu wabunge hao pamoja na wajumbe wengine
wa kikao hicho kushiriki na baadaye kwenda kutembelea miradi ya maendeleo.
Mmbando ndiye liyekuwa Mwenyekiti wa
mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika Jumamosi wiki
iliyopita na baadaye kuhairishwa na kuibua malumbano ya kisiasa.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, hatua
hiyo imetokana na hasira za Ukawa kwa kile kinadaiwa kuwa ni kufanyiwa hujuma
na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi
(CCM) katika kuvuruga utaratibu wa kumpata Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es
Salaam umeghairishwa mara nne mpaka sasa kutokana na kuibuka vuta nikuvute kati
ya Ukawa na CCM huku ikitajwa kwamba, CCM wanaendesha hujuma ili kutwaa nafasi
hiyo licha ya kuwa wachache.
Miongoni mwa wabunge waliogomea
kikao hicho ni pamoja na Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema);
Abdallah Mtulea, Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF); Maulid Mtulia, Mbunge wa
Jimbo la Kinondoni (CUF) na Waitara Mwita, Mbunge wa Ukonga (Chadema).
Wabunge hao wamesema kwamba,
hawatoshiriki vikao vya RCC kutokana na kutokuwa na imani na uongozi wa mkoa.
Kikao hicho kilipangwa kufanyika tarehe 3 Machi mwaka huu katika Ukumbi wa
Kareem Jee, Dar es Salaam.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni