MUSEVENI ASHIKIKI UGANDA,AENDELEA KUBAMBA KWENYE KURA ZA AWALI,SOMA HAPO KUJUA
Yoweri Museveni, Rais wa Uganda, anayetetea kiti chake katika uchaguzi huu |
KINACHOENDELEA kutokea
katika Uchaguzi Mkuu nchini Uganda tangu kukuche leo na kama ilivyoripotiwa na
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ni kama ifuatavyo.
04:37 asubuhi hii: Kiongozi wa waangalizi wa
IGAD Yufnalis Okubo asema kwa maoni ya kundi lake la waangalizi, uchaguzi
ulitimiza viwango vinavyohitajika kimataifa. Ahimiza walioshiriki kukubali
matokeo. Awataka wasioridhika kutumia mifumo ya sheria kulalamika.
04:30 Kiongozi wa
waangalizi wa IGAD Yufnalis Okubo anasema kulikuwa na changamoto katika kuandaa
vituokwa upigaji kura pamoja na kufunguliwa kwa vituo. Asema pia waliona
mabango ya kampeni katika baadhi ya vituo vya kupigia kura. Asema siku ya
uchaguzi, baadhi ya wapiga kura walikosa majina yao vituoni. Wasiojua kusoma
hawakusaidia vyema.
Waliofaa kupaka watu
wino baada ya kupiga kura katika baadhi ya maeneo hawakumakinika sana.
Apendekeza vifaa vya kupigia kura viwe vikifikishwa mkesha wa siku ya kupiga
kura, sawa na kuandaliwa kwa vituo.
04:25 Kiongozi wa waangalizi wa COMESA Ashraf
Gamaal Rashed amesema Tume ya Uchaguzi inafaa kuwezeshwa zaidi ili kutekeleza
majukumu yake vyema.
04:20 Waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki, COMESA na IGAD wanatoa taarifa zao kuhusu uchaguzi. Rais wa
zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi amewapongeza wananchi wa Uganda kwa
kujitokeza kwa wingi. Amesema uchaguzi ulifiofanyika wiki hii ulikuwa na
ushindani mkubwa.
03:59 Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umekanusha
taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa mitandaoni zikiashiria kwamba Marekani
imewaagiza raia wake waondoke Uganda. Ubalozi huo umesema taarifa hizo ni za
uongo.
Matokeo kwa sasa
(Vituo 21,254 kati ya 28,010)
|
||
Abed Bwanika
|
70,708
|
0.95%
|
Amama Mbabazi
|
112,071
|
1.50%
|
Baryamureeba
Venasius
|
42,931
|
0.58%
|
Benon Biraaro
|
20,553
|
0.28%
|
Kizza Besigye
|
2,603,880
|
34.94%
|
Joseph Mabirizi
|
19,661
|
0.26%
|
Maureen Kyalya
|
32,773
|
0.44%
|
Yoweri Museveni
|
4,549,148
|
61.05%
|
Chanzo: Tume ya
Uchaguzi Uganda (EC)
|
02:44 Bw Kiggundu amesema matokeo mengine
yanatarajiwa mwendo wa saa nne, lakini yanaweza yakatangazwa mapema iwapo
yatakuwa tayari. Ametetea tume hiyo dhidi ya madai kwamba kura kutoka ‘ngome za
upinzani’ hayajaripotiwa. Tume inatarajiwa kutangaza matokeo kamili kabla ya
saa kumi alasiri kwa mujibu wa sheria.
02:38 Matokeo yaliyotangazwa sasa hivi ni kama
ifuatavyo. Ni kutoka vituo 21,254 kutoka kwa vituo 28,010. Matokeo
yaliyotangazwa yanajumuisha kura 7,822,737 ambazo ni sawa na asilimia 51,21 ya
wapiga kura 15 milioni waliosajiliwa na tume hiyo. Kumbuka si wapiga kura wote
waliosajiliwa ambao hufanikiwa kupiga kura
02:33 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu anaanza
kutangaza matokeo ya karibuni zaidi.
02:32 Kwa sasa ni wakati wa maombi Namboole,
kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya kwanza ya urais ya karibuni zaidi leo.
02:28 Katibu Mkuu wa chama tawala cha NRM
Justine Kasule Lumumba amekuwa akiwahutubia wanahabari kutoka Bweyogerere
Museveni anaongoza.
NRM inaongoza katika kura za urais na za ubunge na tunasubiri matokeo ya
mwisho. Hata kule mawaziri wameshindwa, ni watu wa kawaida. Waganda waliamua
nani anafaa kuwaongoza. Kwa NRM si habari njema, lakini ni lazima tukubali.
02:13 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa
kuhutubia wanahabari kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda saa sita kasorobo.
02:10 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu ameingia
ukumbini kutangaza matokeo ya karibuni zaidi ya uchaguzi.
01:54 Tume ya taifa ya uchaguzi Uganda
inatarajiwa kutoa matokeo mengine mwendo wa saa mbili asubuhi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni