MGOGORO WA ZANZIBAR WAZIDI MTESA RAIS MAGUFULI,KAULI YAKE YAPINGWA KILA KONA,SOMA HAPO KUJUA
LICHA ya kauli za vitisho zilizotolewa na Rais John
Magufuli wakati akizungumza na wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dar es
Salaam wiki iliyopita kwamba, atawashughulikia watakaoleta fyokofyoko,
Wazanzibari wamepuuza, anaandika Faki Sosi.
Kassim Bakar Ali, Mwenyekiti wa
Jahazi Asilia ambaye pia alikuwa mgombea urais Zanzibar kwenye uchaguzi wa
tarehe 25 Oktoba mwaka jana amesema, Zanzibar ina historia ya migogoro ya
kisiasa.
Amesema,
imekuwa kwenye migogoro ya uchaguzi tangu mwaka 1957 na kwamba, jeshi
halikuweza kuiondoa hivyo kuamini nguvu ama kutumia jeshi ndio muafaka ni
kuchemsha.
Kassim
ameonya kwamba, kutumia jeshi kutachangia kuchochea mgogoro wa kisiasa na hata
kusababisha machafuko visiwani humo.
Amesema
yeye na chama chake hawana imani na jeshi hilo kwa kuwa nao hushiriki katika
kuiba kura “hatunaimani na jeshi kutokana na kuwa wao ni wasisimamizi wa wizi
wa kura.”
Faki
Rashid Maalim Mkazi wa Bububu, Unguja amesema, kilichofanywa na Rais Magufuli
ni kuwatia hofu Wazanzibari na wao wametambua hilo.
“Alitumia
maneno yale kutia hofu tu, lakini hakuna asiyejua kwamba CCM wanaitaka Zanzibar
kwa gharama yoyote lakini pia naamini kwamba, haki hutafutwa na Wazanzibari
wakiamini hilo hawatakuwa na hofu,” amesema na kuongeza;
“Tunajua
ni vitisho tua, hata alipoanza kwa kutaja sijui Dodoma, Nachingwea, Ukerewe
lakini mwisho wa kauli alifikia kwenye kiini chake na kuitaja Pemba na Zanzibar
kwa maana ya Unguja kuwa ndio kuna mateso ya kisiasa.”
Hata
hivyo, Abdallah Kombo Khamis, aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chama
Democratic Part (DP) amesema, kauli ya Rais Magufuli kwamba hausiki na suala la
Zanzibar huku yeye akiwa Amiri Jeshi Mkuu ni kukimbia majukumu.
“Yeye
ni Amiri Jeshi wa Tanzania au wa CCM? kwani amekuwa akikitumikia chama chake
bila kujali maslahi ya wananchi wake,” amehoji Kombo.
Amesema
kuwa, wananchi wa Zanzibar tayari wamezoea kuonewa na kupigwa kama
walivyofanyiwa miaka iliyopita.
“Mimi
mwenyewe ni muhanga wa machachuko na vurugu zilizowahi kutokea miaka iliyopita
kwani nilipoteza kaka yangu kwa kupigwa risasi na askari na mjomba wangu
kupigwa risasi ya mguu mpaka leo ni mlemavu,” amesema Kombo.
Seif
Ali Iddi aliyekuwa mgombea kupita chama NRA amesema kuwa, Wazanzibari wapo
njiapanda kutokana na Rais Magufuli kukwepa kutatua mgogoro wa kisiasa visiwani
humo.
Amesema
kuwa, Rais Magufuli anakwepa kuhusika kutokana na kuwa chama kilichomuweka
madarakani ndicho kinachoshika sukani wa dhuruma visiwani humo huku akibainisha
kuwa, mgogoro wa kisiasa viswani humo ni wa kihistoria
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni