BREAKING NEWS,MAJIPU YATUMBULIWA TENA MDA HUU,ALIYETUMBULIWA JIPU NUSURA AZIMIE MBELE YA WAZIRI,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa
nchi,ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi
wa Umma na Utawala bora,Angella Kairuki amemsimisha kazi mkuu wa chuo
cha utumishi wa umma nchini Said Nassoro kutoka na uzembe uliipelekea hasara serikali ya bilioni 1.
Vilevile
Waziri Kairuki amewasimamisha pia mkuu
wa chuo hicho tawi la Dar es salaam,Joseph
Mbwilo na Silvanus Ngata ambaye
naye ni mkuu wa chuo hicho tawi la Tabora,
Akizungumza
na waandishi wa habari mda huu,Jijini Dar es Salaam,Waziri Kairuki amesema
amefikia hatua hiyo ya kuwasimamisha kazi watu hao ni baada ya kubaini kuwepo
na uendaji usio ridhisha katika vyuo hivyo,
Amesema Nassoro amemsimisha kazi baada ya kushindwa
kuwasimamia watumishi wa chini yake katika chuo hicho na pia kuwa na usimamizi usio na
ufanisi,
Amesema kuwa uzembe huo uliofanywa na Nassoro
umepelekea hadi matawi ya vyuo hivyo kuathirika .
“Mwaka 2011
hadi 2013 bwana Silvanus Ngata aliongeza
gharama za ujenzi wa jengo la chuo cha Mtwara tofauti na ile fedha
iliyopangwa,na hata ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali ilithitisha
ubadilifu huo ,
“Lakini
huyo Nassoro baada ya kugundua kosa hilo alimwamisha bwana
Ngata na kumpeleka tawi la chuo cha Tabora na kuendelea na wazifa wake
na huyo bwana Ngata kutokana na haya hakufuta taratibu pia namsimisha kazi”amesema
Waziri Kairuki,
Pia
waziri Kairuki amesema amemsimamisha Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya
fedha za chuo,
“Huyu Mbwiro kwa mwaka 2013 alitumia vibaya fedha za
ada za wanafunzi za kiasi cha bilioni 1 kwa mwaka fedha mwaka 2014,lakini licha
ya ubadilifu huyo,huyo Nassoro alimteua bwana Mbwiro kuwa Kaimu mkuu wa chuo
kwa upande wa fedha,kwahiyo huyo bwana Mbwiro namsimiasha pia,”amesema Waziri
Kairuki,
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati Waziri
Kairuki anawasimamisha watendaji hao,mmoja wa watendaji hao,Nassoro alikuwepo
kwenye mkutano huo na wanahabari huku akiwa hajui kinatakachotokea,mara baada
ya waziri Kairuki kutaja kumsimamisha kazi,alionekana kama mtu mwenye kupata na
mshangao huo akijizuia hali yake isionekane.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni