NCCR NAO WAIKOMALIA NEC,SUALA LA MITA 200,SOMA HAPO KUJUA
Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura |
“TAMKO lolote
linalotoka kwa mtu yeyote lisilofuata Katiba na Sheria kuhusu mwananchi
akishapiga kura Oktoba 25, halikubaliki,” anasema Faustine Sungura, Mkuu wa
Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa Chama cha NCCR-Mageuzi. Anaandika Hamisi Mguta …
(endelea).
Ni
kauli aliyoitoa leo makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam, akizungumzia
utata unaotumika kutengeneza mazingira ya serikali ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), kutumia nguvu kudhibiti watu watakaobakia karibu na vituo vya uchaguzi
baada ya kupigakura.
Utata kuhusu
umbali ambao wananchi wanapaswa kukaa nje ya vituo vya uchaguzi umeongezeka
baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuamrisha vyombo vya dola kudhibiti wananchi
watakaovunja sheria siku ya uchaguzi. Alisema wananchi wakishapigakura waondoke
vituoni.
Hoja iliyopo na
ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeieleza, na ikatiliwa mkazo na
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, ni kwamba hakuna ruhusa ya
wananchi kukaa vituoni baada ya kupigakura. Tume imesema ni marufuku mpigakura
kubaki ndani ya mita 200.
Sungura amesema
“Kifungu cha 104(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, kinasema
‘hakuna mtu atakayeruhusiwa kufanya mkutano nje au ndani ya kituo wakati zoezi
la uchaguzi linaendelea, au katika eneo la mzunguko lisilozidi mita 200 kutoka
kwenye kituo cha uchaguzi, au kufanya kitu chochote kinachoashiria kumfanyia
kampeni mgombea yeyote’ (tafsiri kutoka lugha ya Kiingereza).”
Sungura amesema
kifungu hicho hakina utata wowote na kwa hivyo anasisitiza, kwa mujibu wa
Sheria ya Uchaguzi “mpigakura hakatazwi kubaki kituoni mara baada ya kupiga
kura na anaweza kuamua kubaki kituoni au ndani ya mzunguko wa mita 200,
isipokuwa anachokatazwa ni kuonesha viashiria vya kumfanyia kampeni mgombea.
“Tuachane na
maneno yote, tuangalie sheria, tunafahamu kuwa mwaka huu ni wa mabadiliko na
hakuna tatizo kwa mpigiwa kura kulinda kura yake na wapigakura kulinda kura za
wagombea wao,” anaeleza Sungura.
Amesema Kifungu
cha 3 cha sheria hiyo kinadhihirisha kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, inawajibu
wa kisheria kusimamia mchakato wote wa mambo ya uchaguzi na kutoa maelezo
kimaandishi yaliyosainiwa na Mwenyekiti au Mkurugenzi wa Tume. Anasema NEC
haikufanya hivyo zaidi ya kutoa tangazo kwenye magazeti.
Sungura amesema
kipengele cha pili kidogo cha Kif. 104 kinafafanua hatma ya makosa ya ukiukwaji
wa Sheria ya Uchaguzi, kikisema, “mpigakura atakayekiuka makatazo
yaliyoainishwa kwenye sheria hii akapatikana na hatia, atapigwa faini ya kiasi
cha fedha kisichopungua Sh. 50,000 na kisichozidi Sh. 100,000.”
Adhabu mbadala
ya kosa hilo ni kifungo cha miezi sita hadi 12 (mwaka mmoja).
Sungura
amefafanua kuwa wao NCCR-Mageuzi wanaona suala la mpigakura kuondoka au kubaki
vituoni lingebaki kuwa hiari ya mpigakura na sio kuamrishwa asikae wakati
sheria haimkatazi.
“Tunachukua
fursa hii kuuarifu umma ya kuwa viongozi na wanachama wote wa NCCR-Mageuzi
wameandaliwa kufuata sheria za uchaguzi na siyo vinginevyo,” amesema.
Anaona kuna
mihemko ya kisiasa na taarifa zilizotolewa isivyo halali kwa kuwa haziendani na
sheria. “Tunaiomba sana NEC isimamie sheria ili uchaguzi ufanyike kwa amani.”
Sungura amesema
pia kuwa kutegemea mawakala peke yao haitoshi hasa kwa kuwa utaratibu
unaotumiwa na Tume ni wasimamizi wa uchaguzi kuwaapisha mawakala wa vyama vyote
kwa siri wakiwa peke yao, hatua isiyoaminika kwa kuwa mazingira yanatoa mwanya
wa kuwatisha au kuwahonga mawakala watumikie maslahi ya CCM.
NCCR-Mageuzi na
vyama vyenzake katika ushirikiano wa Ukawa, vimeelekeza wananchi wabaki maeneo
ya karibu na vituo vya uchaguzi wakishapiga kura ili kulinda kura dhidi ya
kuibwa na kunufaisha maslahi ya CCM waliotangaza kuwa watapata ushindi hata kwa
“goli la mkono.
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni