HABARI KUBWA LEO-MBATIA AMPOPOA DOKTA SLAA,AJIBU HOJA ZAKE ZOTE,SOMA HAPO KUJUA

Mwenyekiti mwenza wa UKAWA
James Mbatia ameongea mchana huu na waandishi wa
habari na kujibu baadhi ya mambo aliyosema Dr. Slaa
Mbatia: Napenda kuwaomba
Watanzania tusimame wote kupata Katiba mpya ambayo ndiyo ajenda ya mgombea wetu
Lowassa. #MbatiaAnaongea
Mbatia: Watanzania naomba
waelewe UKAWA tunasimamia utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji
ndani ya Tanzania.
Mbatia: Wanasiasa hasa wale
wa CCM Mwakyembe na Sita, wanaotaka midahalo waje waongee na mimi wasimsumbue
Mgombea wetu Lowassa sio saizi yao.
Mbatia: Hivi ni ashiria
kwamba CCM wameshindwa hoja, mara kuleta mambo ya udini, mara wanaibua hili
mara lile. wanataka kuchafua amani yetu kwa kuigiza masuala ya dini
Mbatia: Wagombea wetu urais
walikaa na Dokta Slaa alisema mimi ni bora kuliko wote,leo hii anasema hajawahi
kutia nia,kweli?
Mbatia: Tukisema tuibue
masuala yote na kashifa za kuuzwa kwa nyumba, kuna mtu atabaki salama?
Mbatia: Eti Lowassa akija
ndani ya Ukawa atakuja na Wenyeviti wa CCM..hakuwahi kusema..kayasemea wapi?
Mbatia: Wewe unasema ni
muadilifu ulipewa Milioni 500 mwaka 2008 unakuja kusema leo baada ya miaka 7?
Tuwe wakweli.
Mbatia: Eti suala la rushwa
zaidi ya miaka 7 usiripoti halafu uje useme leo, kusema uongo ni kazi sana.
Mbatia: Napenda kuwaomba
watanzania wote ambao ni zaidi ya milioni 46, wasiruhusu nchi yetu ikaharibiwa
na watu 100.
Mbatia: Wakenya walisema
hata kama ana makosa, walisema huyo huyo tunamtaka, wakampigia kura na leo ni
Rais wao.
Mbatia: Watu wachache
wanaotaka eti kwa lolote lile lazima waendelee kubaki madarakani, tunasema
hapana.
Mbatia: Lazima tufute mfumo
huu uondoke tuwe na Tanzania mpya.
Mbatia: Napenda kuwaomba
wale Viongozi wa dini walionewa kwa yale ya jana, wasamehe na waachane nayo.
Mbatia: Lowassa hajawahi
kutamka kuwa nikija ndani ya UKAWA nitakuja na wabunge 50, wenyeviti wa CCM na
Makatibu nk.
Mbatia: Kama hana faida
haya mafuriko tungepata wapi? Nyota ya Lowassa inang'aa hata wafanye nini
hawamuwezi huyu jamaa
Mbatia: Hatuna haja ya
kuanza kumjadili, hiyo ni kulipasua Taifa la Tanzania kwa maslahi binafsi
Mbatia: Kilichotusikitisha
ni yeye kuhusisha watu wengine wasiohusika kwenye jamii yetu, viongozi wa dini
wenye heshima zao, acha sisi vyama vya siasa tusuguane wenyewe.
Mbatia: Zimebaki siku 50 na
kitu, haki itendeki na nchi yetu ibaki na amani siku zote
Mbatia: Anasema kaja
kupambana na Lowassa kwakuwa anagombea urais, sasa Sumaye naye anagombea urais?
Mbatia: Nimesoma barua ya
ufisadi, ufisadi ni mfumo na Lowassa wana haki ya kujielezea zaidi wakitaka
lakini hawa wanataka kututoa kwenye reli tuanze kujibizana mmoja na wengine.
A
Hakuna maoni
Chapisha Maoni