Zinazobamba

DR. FAUSTINE NDUGULILE ALIPULIWA NA MPINZANI WAKE, ADAI AWAAMBIE WANANCHI MIL.450 ZA JIMBO ZIMEENDA WAPI?


MGOMBEA UBUNGE HALALI WA JIMBO LA KIGAMBONI KWA TIKETI YA CHAMA CHA WANANCHI CUF  BW. JUMA SHABANI NKUMBI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA VIJIBWENI WAKATI ALIPOKUWA ANAZINDUA KAMPENI ZAKE ZA KUSAKA KURA KWA JIMBO HILO. NKUMBI ALIWATAKA WANANCHI KUTIA KURA ZAO ZA NDIO KWAKE ILI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI HUMO IKIWAMO FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO.
MGOMBEA UBUNGE WA KATA YA VIJIBWENI KWA TIKETI YA CHAMA CHA WANANCHI CUF. BW SULEIMANI BAKARI MBOGO  AKINADIWA NA KIONGOZI MWANDAMIZI WA CHAMA HICHO KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI ZA MGOMBEA UBUNGE WA JIMBO HILO. SULEIMANI ANASAKA NAFASI YA UDIWANI ILI AWEZE KUWA MWENYEKITI BORA WA KATA HIYO YA VIJIBWENI.

WANANCHI WAKIFUATILIA KWA MAKINI HOTUBA YA JUMA NKUMBI HUKO VIJIBWENI.

NI kama amemlipua!!! Mgombea ubunge wa jimbo la kigamboni kwa ticketi ya chama cha wananchi CUF Juma Shabani Nkumbi amemtaka mbunge aliyemaliza muda wake ambaye pia anawania tena nafasi ya ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM Dr Faustine Ndugulile awaambie ukweli wananchi wa jimbo hilo juu ya fedha za jimbo alikozipeleka.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni zake mapema hii leo, Nkumbi alisema katika kipindi chote cha miaka mitano takribani kiasi cha milioni 450 zimepokelewa na mbunge wa jimbo hilo kwa ajiri ya maendeleo ya wananchgi lakini cha ajabu fedha hizo zimeishia mikononi mwake.

Alisema Dr. Ndugulile hakufanya lolote, kashindwa hata kuanzisha miradi ya vijana jambo ambalo ni sawa na kuwafanyia unyama wananchi wa jimbo hilo la kigamboni

Katika hatua nyingine Mbunge huyo mtarajiwa ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Obama wa Kigamboni amewaahidi wakazi hao wa vijibweni kwamba kama atafanikiwa kushinda chaguzi hizo atahakikisha kero zote za jimbo atazishughulikia.

FAIDI UZINDUZI HUO KWA NJIA YA PICHAA











Hakuna maoni