DOKTA SLAA KUUMBULIWA KILA KONA,TEC WAJIPANGA KUMJIBU ,SOMA HAPO KUJUA
SIKU moja
kupita baada ya Aliyekuwa Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema Dk Wilbroad Slaa kuwatuhumu maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini kupokea
rushwa kutoka kwa mgombea wa Urais kupita Chadema Edward lowassa ,
Ambapo sasa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania (TEC) limechukizwa na tuhuma hizo na mda wowote kutoka sasa
wanajiandaa kutoa tamko kali kwa kupinga tuhumu hizo.
Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu aliyoko ndani ya Baraza hilo ameuambia
mtandao huu kuwa wako mbioni kuweka sawa taarifa hizo.
Amesema TEC hawatafumbia habari zozote zitoelewazo kwa jamii zenye kuleta utofauti wa kimitazamo na kupanga kutoa taarifa ya ukweli ili jamii ijue,.
“Kusema kweli hata hizi taarifa
tumezisikia na sisi,yaani hatutegemea kabisa mtu ambaye anahaminika kama Dk Slaa
kuongea mambo kiajabu kama vile,kama anasema kuna maaskofu 30 wamehongwa ni
vema angewataja,lakini amekaa kimya basi na sisi tutatoa tamko kwenu kuhusu
hali hiyo maana kauli hizi zinakuwa zinautata”kimesema Chanzo hicho.
Dk Slaa ambaye kihostoria aliwai kuwa
Padri wa kanisa Katoliki alitangaza kile anachodai ni kununja ukimwa uliokuwa
umetanda juu ya hatma yake ndani ya Chadema huku akiwaambia waandishi wa Habari
jana kwenye hoteli moja hapa jijini alisema sababu ya kuachana na Chadema
pamoja na kuachana na siasa inatokana kile anachoiita ni kupuuzwa kuhusu hatua ya kumkaribisha Lowassa.
UTATA WA
MKUTANO WAKE NA WANAHABARI.
Mwandishi wa
Mtandao alifika kwenye hoteli ya serena jijini dare s Salaam na kushuhudia
umati wa waandishi wengi ambao tofauti na kawaida,wakati waandishi wa Habari
wakisubili mkutano huo kuanza ,ukumbi Kote Kulizungukwa na watu wanaozaniwa kuwa
ni wa Idara ya Usalama wa Taifa huku ikizidisha mashaka uwepo wa watu wale
pale.
Wakati Slaa
anawasili kwenye mkutano huo aliongoza na Mhariri moja wa Gazeti linalotoka
mara moja kwa wiki huku akiongozana pia na
watu wanaozania kuwa ni usalama wa Taifa waikifikia saba.
Wakizungumia hali hiyo baadhi ya waandishi wa
habari waliokuwepo katika mkutano huo, waliumbia mtandao huu kuwa mkutano huo
uwenda ulikuwa na malengo tofauti ya kisiasa kwani uwepo wa usalama Taifa hao
unatilia shaka.
“Yaani hata
sisi tunashangaa hawa wanaozaniwa ni usalama wa Taifa wapo kwenye mkutano na
wanahabari, harafu wanapigia makofi
anachozungumza Slaa,tena mbaya zaidi huyuhuyu Slaa wakati yupo chadema alikuwa
anawatuhumu watu hawa kuwa walikuwa wanataka kumdhuru,sasa inakuwaje huyu huyu leo analindwa na hawa hawa alikuwa wanatuhumu
watanzania wawe makini”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni