WAZIRI SITTA AMLIPUA ZITTO KABWE,NI KUHUSU RUGEMALIRA,AMESEMA NI MUONGO NA MPOTOSHAJI SOMA HAPA KUJUA
NA KAROLI VINSENT
Siku chache
kupita baada ya Kiongozi Mkuu wa Chama cha siasa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe (pichani) kifichua kile
anachodai ni ufisadi unaofanywa na Serikali kwa kitendo chake cha kumpa tenda Mkurugenzi wa VP
Engineering Bwana James Rugimalira kwenye Ujenzi wa Reli kutoka Mwambani Tanga
hadi nchini Kongo kwa kudai kumegubikwa na ukiukwaji wa kanuni kutokana na kutotangazwa
tenda hiyo kwa umma.
Naye Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta ameibuka
na kumvaa mwanasiasa huyo na kusema amejaa uongo na ni mpotoshaji kwani
serikali haihusika na mradi huo na wala haijatoa fedha kumpa bwana Rugimalira.
Kauli hiyo ya Waziri Sitta ameitoa
leo Jijini Dar es Salaam wa wakati wa Mkuano na waandishi wa Habari ambapo
amesema inasikitisha kuona mwanasiasa anataka kujijenga kisiasa kupitia kwenye
mambo anayodai ni ya uongo,kwani mradi ambao anafanya bwana Rugimalira ni
mpango wakwao kwenye sekta binafsi.
“Kwanza hakuna ufisadi wowote
kinachotokea kule mwambani Tanga ni watu wa sekta binafsi wanabuni mitaji na Rugimalira ndio anafanya hivyo kwa
kushirikiana na shirika la Maendelea (NDC)wanakuwa wanakibuni mitaji baadae kuja kutuletea serikali na sisi tunaweza
kukubali au la”amesema Waziri Sitta
Waziri Sitta ameongeza kuwa kitendo
anachosema kwamba Serikali imehusika kutoa fedha zake sio kweli na amesema uhenda Mbunge huyo wa zamani wa Kigoma alikuwa ataka umaarufu tu wakisiasa.
Amebainishwa kuwa na hata katika hatua
za awali teyari Serikali ilikuwa imeukataa mradi wenyewe wa Reli kwa kuwa
wamebaini hautawezi kuinufaisha nchini kwakuwa sehemu kubwa ya Reli
itajengwa nje ya nchi ambayo ni nchi ya Kongo.
“Harafu tena katika hatua za awali
tumesema hatuwezi kukubali kabisa kuhuruhusu huo mradi tuuchukue serikali kwani
hatuwezi kunufaika nao kwakuwa sehemu kubwa ya reli inajengwa nje ya nchi na
sehemu ndogo tu ndio tunanufaika watanzania achia mbali sehemu ndogo pia sisi
tayari pale tanga kuna Reli ipo hatuwezi kuuchukua mradi huo “amebainisha
Waziri Sitta.
No comments
Post a Comment