UKAWA WAANZISHA KIVUMBI BUNGENI,SPIKA AHAIRISHA BUNGE,SOMA HAPA KUJUA
SPIKA wa Bunge-Anne Makinda, amelazimika kulihairisha Bunge kwa
dharura hadi hapo baadaye kutokana na wabunge wa upinzani kutoka vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutaka Serikali itoe ufafanuzi
kuhusu uandikishaji wa wapiga kura kwa mfumo wa BVR unaoendelea…Anaripoti
Mwandishi Wetu …
(endelea).
Kizaazaa hicho kiliibuka baada ya Mbunge
wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) kuomba mwongozo wa Spika akitaka Bunge
lisitishe shughuli zake na kujadili suala hilo la dharura kwa sababu hadi sasa
hakuna mkoa uliomaliza kuandikisha wapigakura na hivyo kuleta utata kuhusu kura
ya maoni ya katiba pendekezwa iliyopangwa kufanyika 30 Aprili mwaka huu.
Baada ya Mnyika kutoa hoja hiyo
huku akizomewa na wabunge wengi wa CCM, Spika Makinda alisema kuwa suala hilo
haliwezi kujadiliwa kwa sababu linafanana na lile la kuifanyia marekebisho
katiba ya sasa lililokuwa limehojiwa na mbunge mwingine, kwamba yote kwa pamoja
yangetolewa majibu na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo jioni wakati wa hotuba
yake ya kuhairisha Bunge.
Hata hivyo, uamuzi wake
haukukubaliwa na wabunge hao wa Ukawa ambao kwa pamoja walisimama na kuanza
kupiga kelele wakisema “tunataka majibu…majibu kwanza mengine baadaye…Waziri
Mkuu yupo pale atoe majibu”.
Kelele hizo ziliendelea kwa
takribani dakika saba na licha ya Spika kulazimisha Katibu wa Bunge kusoma ratiba
ya utaratibu unaofuata, bado hakufanikiwa na hivyo kutangaza kuliahirisha Bunge
kwa muda usiojulikana hadi hapo baadaye.
Endelea kufuatilia mtandao huu utapata mkasa wote
No comments
Post a Comment