Zinazobamba

SINEMA YA ASKOFU GWAJIMA YAZIDI ENDELEA,APANDISHWA MAHAKAMANI,SOMA HAPA KUJUA



Asubuhi ya leo imeripotiwa stori ya Askari Polisi wakiwa na silaha kuizunguka nyumba yake, Mbezi Salasala DAR.. waumini wake, waandishi wa habari pamoja na watu wengine walikuwa pembeni pia, kuangalia kinachoendelea.
Muda mfupi baadae imeripotiwa kwamba Askofu huyo alienda Kituo cha Polisi Centre lakini haikuchukua muda mrefu akatolewa na kupelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu DAR.. 
Taarifa  kutoka  Mahakamani  zinaarifu  kuwa Gwajima  amepata dhamana na atarudi mahakamani hapo Mei 4, 2015. 
Josephat Gwajima ameshitakiwa kwa makosa mawili ambayo  ni kutoa lugha ya matusi na kushindwa kutunza silaha.
  HIVI NDIVYO KULIVYOKUWA NYUMBANI KWAKE MWANADISHI
 WA MTANDAO HUU KAROLI VINSENT ALIKUWEPO NYUMBANI HAPO
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA

 Askari wakiwa nyumbani kwa Gwajima.
 Makamanda wa polisi wakiwa tayari kwa lolote.
 Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano.
 Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio.
 Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.
 Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba wa askofu wao.
 Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwake mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
 Baadhi ya watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Gwajima wakichungulia dirishani.
 Baadhi ya waumini wa Gwajima wakifuatilia kwa makini hali iliyokuwapo.
 Baadhi ya waumini wakiwa mbele ya nyumba ya Gwajima.
 Gari la polisi likiondoka eneo la tukio.
Hapa wakishangilia ushindi baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.

No comments