HABARI KUBWA LEO-BAKWATA WAPINGANA NA MAASKOFU,TAASISI YA KIISLAM,WAUNGANA NA SERIKALI,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mkuu wa Bakwata mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhad Mussa Salum Picha na Maktaba |
BARAZA la
kiislam nchini (BAKWATA) limewataka waamini wote wa dini ya kiislam nchini
kuisoma Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba kuielewa na kuipigia
kura ifikapo tarehe 30-april kwaka huu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kauli hiyo ya BAKWATA inakwenda tofauti na Mwamvuli wa Jukwaa la Wakristo Tanzania,
ambalo ni pamoja la Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la
Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) ambao wao walitoa tamko ambalo
limesomwa kila kanisa wiki hii-
Likiwataka waamini wa dini ya kikristo kupigia kura ya Hapana katiba
iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
Mbali na maaskofu Bakwata wamekwenda
tofauti na Jumuiya ya Taasisi za kiislam nchini ambao nao wamewataka pia
waamini wa dini hiyo kupigia kura ya hapana katiba hiyo kama haitoitambua
Mahakama ya Kadhi.
Kauli ya Bakwata imetolewa mda huu
jijini Dar es Salaam,na Mkuu wa Bakwata mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhad
Mussa Salum wakati wa Mkutano na Waandishi Habari pamoja na mambo mengine amesema kwa sasa wao Bakwata hawezi kuwataka
waislam nchini kuipigia kura ya hapana katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum
la Katiba.
“sisi tumewataka waamini wa dini ya kiislam
nchini kuisoma kwa umakini katiba iliyopendekwa na Bunge maalum la Katiba na
ikifika wakati wa kupigia kura waamue wenyewe,maana sisi hatuwezi kuwalazimisha
sisi kupigia kura hapana kama wanavyofanya wengine”amesema Sheikh Salum.
Sheikh Salum ameongeza kuwa kwa kuwataka
waislam nchini kuitafuta katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum,
Katika
hatua nyingine Sheikh Salum ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Amani amemvaa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi
CCM,Mh Abdurahman Kinana kutokana na
kitendo chake cha kumshambulia Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu
kwa kumwita waziri huyo ‘eti anazurula tu na wala afanyi kazi yoyote na kwamba
anathamini wanyama kuliko binadamu”
“Kamati ya amani imesikitishwa sana na kauli za kinana ambazo zinalengo kumbeza waziri
nyalandu katika jitihada zake anazochukua katika kupambana na majangili wa
wanyama ambao wamekuwa wakimaliza wanyama”Ameendelea kusema Sheikh Salum.
Aidha
Sheikh Salum amemtaka katibu huyo wa CCM kuacha kumbeza Waziri Nyalandu na
akamtaka kuwaangali wakuu wa wilaya pamoja na mikoa ambao wamekuwa na tabia ya
kuzurula bila kuwa na mipango yoyote.
Kamati hiyo ya Amani ambayo inaongozwa na
Mwenyekiti Sheikh Salum pamoja na kuundwa na viongozi mbali mbali wa dini ya
kikristo pamoja na dini ya Kiislam.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni