KIFO CHA KOMBA,WANASIASA WAMLILIA,DOKTA SLAA ASEMA YAMOYONI,SOMA HAPA KUJUA
SAA chache
kupita baada ya Mbunge wa Mbinga mashariki Kaptain John Komba kufaliki Dunia Gafla
kutoka na kusumbuliwa na Ugonjwa wa kisukari kwa mda mrefu , Viongozi
mbalimbali wakimwemo wanasiasa wametoa masikitiko yao kufuatia kifo
hicho.Anaripoti KAROLI
VINSENT endelea nayo
hapo.
Wakizungumza na Blogs hii kwa
wakati mmoja wanasiasa hao wameonyesha kugushwa na msiba huo, na Wakwanza
aliyezungumza na mwandishi wa Habari hii ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa amesema kifupi yeye mwenyewe amepata
taarifa hizi kupitia mitandao ya kijaa
na imemsikitisha sana.
“Kikukweli mimi mwenyewe nimepata taarifa hizi
kwenye mitandao mbalimbali cha kwanza imenisikitisha sana,kwani Komba ni
miongoni mwanasiasa waliolijenga taifa hili changa kwa mafanikioa makubwa sana”amesema
Dokta Slaa.
Dokta Slaa ameongeza kuwa anatumia nafasi hii kutoa pole kwa Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Jakaya Kikwete
ambacho ndicho chama Komba
anatoka kwa msiba huo mkubwa, na akawataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki
kigumu.
Naye Mwenyekiti asiyetambulika na
Msajili wa Vyama vya Kisiasa nchini kutoka chama cha ACT-Tanzania Kadawi Limbu
naye ametoa pole kwa chama cha Mapinduzi CCM kwa msiba huo pamoja na Wasanii
kwa ujumla na akisema Taifa maendeleo.
Kwa Upande wake Mwandishi wa Habari
Mwandamizi kutoka kituo Cha Chanel Ten pamoja na Radio ya Magic Fm Kibwana
Dachi naye ameonyesha masikitiko yake baada ya kutokeo kwa kifo hicho na Kusema
ni pigo kubwa sana kwa Taifa.
“ Kifo cha Komba kimenisikitisha sana na hata kwa watanzania
wote hususani sisi waandishi wa habari kwani ni mtu aliyeijenga jamii ya kisiasa kwa kutumia maono
mazuri,na hata pia katika sanaa ni mtu aliyerudisha mfumo wa uimbaji kwa
kutumia mfumo wa kwaya yaani kwa kifupi naweza kusema ni pengo kubwa sana kwa
taifa”amesema Dachi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni