HABARI KUBWA LEO-PINDA HAFAI URAIS,YAELEZWA NI MTU HATARI SANA,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mizengo Pinda |
MIZENGO Pinda, waziri mkuu wa Jamhuri, hafai urais. Hapaswi
kufikiriwa kuwa miongoni mwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaoweza
kupendekezwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho. Anaandika Pendo Omary
…(endelea).
Kinachomuondoa Pinda katika
mbio za kusaka urais, ni kauli zake za kibabe dhidi ya wananchi; kushindwa
kusimamia serikali na lundo la kashfa linalomkabili.
Waziri mmoja mwandamizi serikalini
amesema, “ni hatari kwa taifa hili kukabidhiwa mwanasiasa anaina ya Mizengo
Pinda.”
Amesema, “Tumefika hapa kwa
sababu ya udhaifu wa Pinda. Huyu bwana ameshindwa kusimamia serikali. Ni dhaifu
anayetaka kuvitumia vyombo vya dola kulinda utawala wake.”
Akiongea kwa uchungu, waziri huyu
amesema, “Tangu amekuwa waziri mkuu Pinda ameponyoka katika kashfa karibu nne
huku walio chini yake wakitakiwa kujiuzulu.”
Kashfa ambazo Pinda amenyoka, huku
mawaziri wake wakiangamizwa kisiasa, ni pamoa na ukwapuaji mabilioni ya
shilingi katika Akaunti ya Escrow na operesheni tokomeza.
Pinda ndiye aliyeagiza jeshi
la polisi kupiga raia kwa kile alichoita, “serikali imechoka kuvumilia.”
Kauli ya Pinda ni kuvunja Katiba ya
Jamhuri ya Muungano inayopiga marufuku katika Ibara ya 12 kwa mtu yeyote
kuteswa ama kuadhibiwa kinyama na kumpa adhabu, ambazo zinamtesa mtu na
kumdhalilisha.
Pinda aliliambia Bunge mjini Dodoma 20
Juni 2013, “…umeambiwa usifanye hiki, wewe ukaamua kukaidi, utapigwa tu.”
Alikuwa akijibu swali la mmoja wa
wabunge aliyetaka kujua “vitendo vya vyombo vya dola kupiga raia mkoani
Mtwara.”
Alisema, “Ukifanya fujo,
utapigwa tu. Maana hakuna namna nyingine. Maana lazima wote tukubaliane kwamba,
nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.”
Alisema, “Sasa kama wewe
umekaidi, hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndiyo jeuri zaidi,
watakupiga tu. Na mimi nasema muwapige tu. kwa sababu hakuna namna
nyingine. Maana tumechoka sasa.”
Kuibuka kwa waziri huyo mwandamizi
kudai Pinda amepoteza sifa ya kuwa rais; na kumtuhumu kuvitumia vyombo vya dola
kulinda udhaifu wa serikali, kumekuja wiki moja tangu jeshi la polisi
kumshambulia na kumdhalilisha mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof.
Ibrahim Lipumba.
Prof. Lipumba alidhalilishwa wakati
akielekea eneo la Zakhem, Mbagala, kuhutubia mkutano wa hadhara uliolenga
kuwakumbuka mamia ya wafuasi na wanachama wa chama hicho, waliouawa na polisi
Januari 26 na 27 mwaka 2001.
“Kama mtu amechoka kuongoza,
huomba kupumzika. Kutumia vyombo vya dola kulinda udhaifu wako, ni kutaka
kuingiza nchi katika machafuko. Hakukubariki,” ameeleza waziri huyo ambaye
ameomba kutotajwa jina lake.
Pinda anatajwa kuwa miongoni mwa
wanachama wa CCM walioamua kutafuta urais kufa au kupona.
Mbunge wa Singida Mashariki
(Chadema), Tundu Lissu amesema, Pinda siyo kwamba hakuhusika na kashifa ya
Escrow, bali aliondolewa kutokana na kuwapo maridhiano.
“Wabunge wa CCM waliapa
kutounga mkono mapendekezo ya Bunge. Waliweka sharti la kuondolewa Pinda.
Walifanya hivyo ili kulinda serikali na Jakaya Rais Kikwete,” ameeleza Lissu.
Taarifa zinasema, wabunge hao
wakiongozwa na Anne Kilango Malecela, walidai kuwa hawatapenda kumuona Rais
Kikwete anakuwa na mawaziri wakuu watatu katika utawala wake wa miaka 10.
“Katika makubaliano hayo, ndipo
unaona hata katibu mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, naye anatolewa. Tuna
ushahidi kwamba huyu bwana ndiye alikuwa anashinikiza fedha za Escrow kulipwa.
Lakini tumeshindwa kumwajibisha kwa sababu ya tabia ya kulindana ya CCM,”
ameeleza Lissu.
Chanzo Ni
Gazeti la mwanahalisi Online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni