DC MAKONDA AANZA KAZI KWA MIKWALA MIZITO SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda |
MKUU mpya wa
wilaya ya Manispaa Kinondoni Paul
Makonda ameapa kufa na matajili pamoja na viongozi mbalimbali waliovamia maeneo
ya wazi na kujimilikisha kinyume na sheria.Anaandika KAROLI VINSENT Endelea
nayo.
Makonda ameyasema hayo leo Jijini Dar
es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari mara baadya ya
kukagua shule za msingi zilizopo kata ya Tandale Ambapo Makonda amesema hatokubali
kuona watu wanaojiita matajili ambao wameshirikiana na viongozi wa
Halmashauri katika kuwapora wananchi
maeneo ya wazi na kujimilikisha huku wananchi wakihangaika .
“Nawapa salam kabisa viongozi wa
Halmashauri ambao wameshirikiana na
matajili ili kupora maeneo ya wazi ambayo yapo kwa
ajili ya viwanja vya michezo lakini viongozi warafi wa halmshauri wameona
sahihi kuwapora viwanja,nasema sitokubali
kabisa,nawapa salam lazima viwanja virudi na atakaye kaidi basi nitakuja
kuvunja na polisi wangu”amesema Makonda.
Makonda ameongeza kuwa tatizo la
migogoro ya Ardhi ataliweka kipaumbele katika wilaya hiyo ili kuweza kumaliza
na ikiwezekana kuondokana na tatizo hilo.
Aidha,Makonda amewataka wananchi wa
manispaa ya kinondoni wampe ushirikiana ili kuweze kuiweka manispaa hiyo katika
hali nzuri ya kimaendeleo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni