WAHARIRI WA HABARI WAPEWA SOMA NA MAAFISA UHUSIANO WA SERIKALI SOMA HAPA KUJUA
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Robert Hokororo wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini Leo Mjini Mtwara.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwaeleza jambo Maafisa Mawasiliano Serikalini kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wa kikao kazi hicho Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wa kikao kazi hicho Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwaeleza washiriki wa Mkutano huo umuhimu wa kuelimisha umma kuelekea upigaji kura ya maoni na kuwataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza suala hili la kitaifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JL Communication inayochapisha magazeti ya Jambo leo na StaaSpoti Bw. Theophil Makunga akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara pia aliwataka Maafisa Mawasiliano kutengeneza mazingira yatayowezesha kufanya kazi na wanahabari.
Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini leo Mjini Mtwara
Baadhi ya Maafisa Mawasiliano wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini leo Mjini Mtwara
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi(MUHAS) Dkt.Ave Maria Semakafu akiwaeleza jambo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara(mwenyekoti jekundu) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga
Katibu wa Jukwaa la Wahariri akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini leo Mjini Mtwara.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) Bw. Innocent Mungy akiwasilisha Mada kwa washiriki wa Mkutano huo kuhusu wajibu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini katika kuimarisha mawasiliano ya serikali kwa umma.
Mjumbe wa Jukwaa la wahariri Bw. Salim Salim akiwaeleza washiriki wa mkutano huo Umuhimu wa kuwa na Usiri katika utendaji kazi (Picha na Hassan Silayo)
Hakuna maoni
Chapisha Maoni